Hii imekaaje?

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,440
Reaction score
38,437
Morning wana JF!

Mwenzenu kuna kitu kinanipa shida akilini! Naamini wengi wa members humu hawafahamiani kwa sura! Humu JF mimi kila siku najihisi kama nawasiliana na watu ambao tunafahamiana vizuri, yaani akili yangu inawaza kwamba watu wa humu tunajuana, haitaki kukubali kuwa wana-JF hawajuani kwa sura! Bahati mimi nilikutana na Mwana-JF mmoja tu, tena mara 1 tu, kuna biashara ilikuwa tufanye lakini hatukufikia muafaka! Kuna baadhi ya posts huwa zinafurahisha, zingine zinahuzunisha, mimi hizi huwa zinanipa hisia kuwa hawa watu wapo karibu sana! Hata michango ya members pia, kuna wakati nacheka, kuna wkt naumia, naamini kabisa kuna ukaribu, japo kwa macho nakataa!
Zaidi ya huyo, sijawai kukutana na member yeyote yule wa JF!

Hii hali inaniathiri hata ninapotaka ku-post uzi wwt ule, najikuta natumia muda mwingi sana wa kufikiria kuwa nitume ama nisitume! Kwa mfano last week nilipost kuhusu uhusiano wangu na mzee, unaweza usiamini, ule uzi niliuandika na kukaa nao kwa muda wa wiki 3, kabla sijaamua kuupost!

Jamani hili kama ni tatizo, tunaliitaje? Ni nini hiki?
 
Ni kweli wengi wetu hatujuani.mimi niko huku liberia ila nafeel kama niko bongo nikiingia jf.
 
Jamani hili kama ni tatizo, tunaliitaje? Ni
nini hiki?

Sio na wala hakuna tatizo lolote.

Huenda nafsi yako inapenda sana marafiki au ni nyepesi sana kuamini na kuaminishwa au maisha yako upande wa pili ni ya upweke na hapa ndipo uonapo patoa faraja kwako.
 
unataka kusema nini,, tusichoshane weekend hii.,
em sema unataka sema nini.
 
Jf ni kijiwe murua sana we tambua hilo tu ukiwa mpweke njoo huku uburudike

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
mmh Afu we slim ujue leo nimekuotaota kama!
 
Hakuna tatizo mkuu . Maana mgefahamiana hapa sidhani kama ungekua na uhuru wa kopost kile unacho kiitaji.. lazim ungekua unastack stak kufikiria ivi flan ataniionaje bt now uko free. Ila ukipata atakae penda mfahamiane sio mbaya pia
 
Imekaa vizuri sana haina tatizo kabisa, JF is the free stress zone, ni sehemu ya kuburudika na kujifunza, hii ni fasihi andishi yaani unajisikia uko karibu kabisa na hadhira yako.
 
Aisee! Jf pametulia sana hata uwe na stress vp lakin hapa ni mwisho wake......... Japo siku moja jf ilitaka kunivunjia mahusiano na bibie wangu kwasababu kila akiuliza mm nilikuwa simjibu nilikuwa bize kuchat na members ikabidid afuatilie post zang zote
 
Wewe unashida binafsi!kwani kujuana na mtu ni kosa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…