Basi mama olewa nae. Hawa wanakuonea tu maana hawajui jinsi ulivyo desperate.
Angalia maandishi mekundu halafu ulinganishe na haya maneno yako
"Kwa mda sasa kulikuwa na minong'ono ofisini kuhusu mahusiano yake ya siri na rafiki yangu wa kike ambaye kwa kipindi chote hicho alikua ametengana na mume wake. Ukweli ni kwamba hakuna mtu ambaye alikua na uhakika kuhusu mahusiano yao ila kulikuwepo na viashiria kwamba mahusiano yao yalikua zaidi ya "just casual friends".
Kila watu wanapojaribu kumtathmini huyu jamaa we unamtetea. Huyu jamaa wakati anatoka na rafiki yako wewe ulikuwa ofisi hiyo hiyo na alikuwa anakuona kila siku, na alikuwa anajua hataweza kumuoa rafiki yako. Iweje leo ndo akufate akwambie we ndo mke mwema na anataka ndoa by mwaka kesho??? This jamaa is very intelligent, very playful. Amekuangaliaaa, akajua unachotaka kuskia - ndoa. Na alijua utahoji kuhusu uhusiano wake na shogako, akaku-pre-empty. We ukamuona shujaa kwamba eti ame-confess! wewe! Linda sana moyo wako kuliko vyote ulindavyo....... Au kama vipi huu ushauri kamuombe rafiki yako.