Miss Kim
Senior Member
- May 3, 2014
- 164
- 273
Kwanza nitangulize salamu wakuu. Natumai wote wazima wa afya. Ni hivi,kuna huyu kijana ambaye ni workmate na tumeshafahamiana kwa miaka 4 sasa. Kwa mda sasa kulikuwa na minong'ono ofisini kuhusu mahusiano yake ya siri na rafiki yangu wa kike ambaye kwa kipindi chote hicho alikua ametengana na mume wake. Ukweli ni kwamba hakuna mtu ambaye alikua na uhakika kuhusu mahusiano yao ila kulikuwepo na viashiria kwamba mahusiano yao yalikua zaidi ya "just casual friends".
Sasa huyu rafiki yangu mume wake amemrudia na kuomba radhi na tayari mipango ya ndoa imeshaanza. Harusi yao ni mwishoni mwa mwaka huu na vikao vimeshaanza. Sasa hapa ndo tatizo langu linapokuja. Yule kijana ambaye alikua anahisiwa kutoka na rafiki yangu alinifuata na kuniambia ukweli,kwamba ni kweli walikua na hasiano ya kimapenzi ila kwa siri kubwa sana kwasababu mume wake na rafiki yangu ni mtu mwenye hela sana na angefanikiwa kutambua chochote kuhusu mahusiano yao angeweza hata mtenda vibaya yule kijana. Ila sasa kwa kuwa rafiki yangu anaolewa anaona hana budi kutafuta mwanamke mwingine kwasababu na yeye mipango yake ni kuoa na kuanzisha familia yake by next year.
Mm nikamuuliza swali rahisi sana,kwanini mimi? Akasema kwasababu nakufahamu na ni mwanamke ambaye ningependa awe mke wangu. Nikamuuliza,je kuhusu mahusiano yako ya siri ya rafiki yangu? Akasema hiyo itabaki kuwa siri kati yetu wawili (yy na rafiki yangu). Ila kusema kweli wakuu mm binafsi nahisi hii haijakaa vizuri kwa sababu tayari nimeshafahamu kwamba jamaa alikua anatoka kimapenzi na rafiki yangu tenda kama ndugu yangu halafu leo hii mm nije kutoka naye? Yeye anasema haina shida kwa sababu hakuna aliyekua anajua kuhusu mahusiano yao,ila je rafiki yangu atanichukuliaje? Na pia najiuliza inamaana huyu kijana kaniona mm ndo "rebound love" yake?
Msaada kwenye tuta wakuu. Asanteni kwa mawazo na ushauri wenu.