Hii imekaaje wakuu?

Hii imekaaje wakuu?

Kuna hii hali ya ndugu na marafiki wanakuja kwako kukuomba hela, ila kwa kuona ili asiendelee kuwa ombaomba pamoja na kuwa na maisha magumu, unaamua kumpa kazi kwenye biashara zako au kampuni.

Matokeo yake anakataa kazi na kulalamika ya kuwa, umeshindwa kumsaidia.

Hii imekaaje wakuu?, Na wahenga wanasema, ‘Mtu akikuomba samaki usimpe samaki bali mfundishe namna ya kuvua samaki.”​
Huyo unaachana naye na hata nauli ya kurudia alipotoka hapati, lakini to be fair isije ikawa mtu mzee au mgonjwa unampa deal kama hiyo, haifai, wengine hawawezi tena kufanya kazi ni kusaidiwa
 
Toka mwaka juzi mimi, niliweka nadhiri ya kutomhusisha ndugu kwenye biashara zangu! Kama ikitokea basi sio kwenye nafasi za maamuzi "decision making".... fedha na mipango. Kuna ndugu mmoja wa kuja, juzi kati tuu hapa akauza mpango kwa mshindani "competitor" ... iliniathiri sio kidogo.
Emagine! Mtu ni in charge wa biashara, anafanya partnership/sidelining ya siri na competitor. Manipulation was well orchestrated, nilipochukua hatua ya kumpiga chini, akaenda upande wa adui... disrespect was unbelievable....!!
Usiniulize nilifanikiwa vipi kurudi njiani tena na biashara ile,,, itakusisimua....
Hii inatafsiri kwa sisi weusi, ukifanikiwa ndugu na wale wakaribu yako wanakuwa wanapambana ili kukushusha, je na kwa wenzetu iko hivyo?
 
Huyo unaachana naye na hata nauli ya kurudia alipotoka hapati, lakini to be fair isije ikawa mtu mzee au mgonjwa unampa deal kama hiyo, haifai, wengine hawawezi tena kufanya kazi ni kusaidiwa
Unakuta wana nguvu kabisa, wakati mwigine kazi wanazofaya unaona kabisa haziwafikishi mbali, unaona bora uwasogeze karibu wafanye kazi waweze kula mema ya dunia, wao hawataki kuwa chini yako.​
 
10,000x365= 3,650,000… mpe hiyo kama unayo alaf mpe maelezo yake
Ki-ujasiriamali unaitoa hiyo kutoka wapi, na pale ulipoipunguza itarudije? Kama mikopo n.k inakuja na riba, je hiyo utakuwa umeamua kuitupa tu?
 
Hii inatafsiri kwa sisi weusi, ukifanikiwa ndugu na wale wakaribu yako wanakuwa wanapambana ili kukushusha, je na kwa wenzetu iko hivyo?

Wanaweza wasiwe wanapamba kukushusha, lakini mindset zao za kukosa shukrani na tamaa, zinaweza kuingia hapo katikati. Watu weusi tuna shida sana ya "mindset". Shida kubwa sana.
 
Back
Top Bottom