Hii imekaaje? Virusi vya ukimwi vyanichanganya!!

Redey

Member
Aug 18, 2009
47
4
Tumeoana miaka mitano iliyopita, mara baada ya kuoana mmoja kati yetu alifanya HIV test na kugundua yuko reactive, bila kumshirikisha mwenzi wake kwakuamini kuwa yeye ndiye chazo. Hivi majuzi tumeenda wote kwenye VCT centre na ikabainika kuwa mmoja kati yetu ni nonreactive na mwingine ni reactive. Cha kushangaza ni kwamba mda wote huu hatujawahi tumia kinga. Sasa ni nini kinamfanya mmoja kuwa non-reactive wakati tumeishi miaka mitano kwenye hii hali?
Naomba nieleweshwe nini kinasababisha. Wataalam nawategemea mnieleweshe.
 
kwa uelewa kidogo, nadhani wakati wa tendo la ndoa michubuko haikutokea ndo maana mkapunguza uwezekano wa 1 wenu kuambukizwa
 
Yah!`Michubuko ndy reason I think... Inaelekea huwa mnaandana vema kiasi kwamba lubricant inakuwa tele kwenye chungu
 
Kuna matatu,

1. Kama walivyosema wengine, inawezekana hakuna mchubuko uliosababisha maambukizi.Ingawa kama mnakutana hata mara moja kila wiki mbili kwa miaka miano ni vigumu kutopata mchubuko, labda uniambie mmetumia mpira muda wote, kitu ambacho haielekei kuwa kilitokea kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa.

2. Inawezekana umeambukizwa lakini kinga yako ni kali sana na virusi ni vidogo sana kiasi havionekani.

3. Inawezekana una natural immunity na virusi haviwezi kukuambukiza. Watu wa kundi hili wanatafutwa sana kwa research. Jaribu kuongea na research teams wanaweza kukuchunguza zaidi.Inawezekana ufunguo wa dawa au chanjo ya AIDS unayo.
 
Tumeoana miaka mitano iliyopita, mara baada ya kuoana mmoja kati yetu alifanya HIV test na kugundua yuko reactive, bila kumshirikisha mwenzi wake kwakuamini kuwa yeye ndiye chazo. Hivi majuzi tumeenda wote kwenye VCT centre na ikabainika kuwa mmoja kati yetu ni nonreactive na mwingine ni reactive. Cha kushangaza ni kwamba mda wote huu hatujawahi tumia kinga. Sasa ni nini kinamfanya mmoja kuwa non-reactive wakati tumeishi miaka mitano kwenye hii hali?
Naomba nieleweshwe nini kinasababisha. Wataalam nawategemea mnieleweshe.

Wewe;

  1. Yupi kati yenu ni reactive
  2. Je ni huyohuyo amekuwa reactive tangu mwanzo? au kumetokea mabadiliko?
  3. Mmeshacheki kwa vipimo vingine vya juu au mnatumia rapid test alone?
  4. Mmepata watoto?
  5. Nao status zao zikoje?
Ukitoa hayo, itasaidia zaidi
 
Wewe;

  1. Yupi kati yenu ni reactive
  2. Je ni huyohuyo amekuwa reactive tangu mwanzo? au kumetokea mabadiliko?
  3. Mmeshacheki kwa vipimo vingine vya juu au mnatumia rapid test alone?
  4. Mmepata watoto?
  5. Nao status zao zikoje?

    Mke yuko reactive, na tatizo limegudulika wakati wa ujauzito wa miezi 2. Mtoto kwa sasa anaumri wa miaka 3.5, afya yake ni nzuri. Vipimo tulivyotumia ni test za kawaida. Tumepima zaidi ya hospital tano tofauti kwa nyakati tofauti lakini mjibu ni yaleyale. Kwa kipindi chote hiki cha mmoja kutofahamu chochote, tulikuwa tunavinjari pekupeku kwa zaidi ya miaka minne.
 
Kuna matatu,

1. Kama walivyosema wengine, inawezekana hakuna mchubuko uliosababisha maambukizi.Ingawa kama mnakutana hata mara moja kila wiki mbili kwa miaka miano ni vigumu kutopata mchubuko, labda uniambie mmetumia mpira muda wote, kitu ambacho haielekei kuwa kilitokea kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa.

2. Inawezekana umeambukizwa lakini kinga yako ni kali sana na virusi ni vidogo sana kiasi havionekani.

3. Inawezekana una natural immunity na virusi haviwezi kukuambukiza. Watu wa kundi hili wanatafutwa sana kwa research. Jaribu kuongea na research teams wanaweza kukuchunguza zaidi.Inawezekana ufunguo wa dawa au chanjo ya AIDS unayo.
Bluray!
Hiyo point ya pili nina mashaka nayo saana. Immunity (kinga) na kuonekana kwa virus ni vitu tofauti kabisa. Si kweli kama mtu anaimmunity kubwa anaweza kusababisha maambukizi yasionekane bali immunity inatengeneza reaction (mambo ya antibody and antigen) na hivyo kumprotect mtu from disease. Mie si mtaalam wa biology but that is what I remember. Na kwa structure ya virus wa ukimwi kuanzia life cycle yake sinahakika km uko sahihi.
Kwahiyo please ninashauri mambo ya kiafya tuwaachie wataalam maana jamaa anaweza kuendelea bila tahadhari akapata maambukizi. hapo mie nakubaliana nawaliosema ile fluid inakuwa nyingi then hakukutokea friction. Jamaa anapaswa achukue tahadhari kwa kushauriana na mwenzi wake.
 
Mbona unajicontradict? Unasema mambo ya afya tuwaachie wataalamu, unasema wewe si mtaalamu halafu unaleta opinion zako zisizo na utaalam?

Unajua maana ya immunity? Unajua immunity system inavyofanya kazi?

Unajuaje kama mie si mtaalam?
 
Back
Top Bottom