Hii imekaaje... "mamaa anapokwenda masomoni..." | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii imekaaje... "mamaa anapokwenda masomoni..."

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kibunango, Mar 10, 2009.

 1. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Eti mke kwenda masomoni na mume kubaki analea watoto, ni hujuma au!

  Mpenzi msomaji, lipo jambo moja ambalo nimelinasa likilalamikiwa na
  baadhi ya kinababa. Linahusu wimbi la kinamama kuanzisha mchakato wa
  kujiendeleza kielimu katika vyuo mbalimbali vya hapa nchini na hata
  ng`ambo.

  Juhudi hizo kwa upande mmoja zinaonekana ni njema, lakini kwa upande
  mwingine ni aina fulani ya hujuma. Kwanini muonekano huo ulete
  utatanishi? Vuta subira msomaji wangu nikumegee vionjo.

  Ni kawaida katika baadhi ya familia zetu, baba kwenda masomoni na
  kumuacha mkewe na watoto nyumbani.

  Kadhalika hali iko hivyo kwa kinamama wanaopenda kujiendeleza
  kutafuta vyuo viwe vya ndani ya nchi au hata nje kujiweka katika
  ufahamu wa juu zaidi kitaaluma.

  Wapo wanaolazimika kujiendeleza chini ya taratibu za kule
  wanakofanyia kazi au wengine hujitegemea katika kujigharimia
  kimasomo.

  Swali ni je, pamoja na nia hiyo nzuri, ipo harufu yoyote ya hujuma
  kwa maana ya uvunjifu wa uaminifu watu hawa wawapo masomoni?

  Hivi majuzi nilikutana na kinababa fulani wakawa wanaelezea wasiwasi
  kuhusu wimbi la kinamama walioolewa kuonekana wakijizatiti kwenda
  kusoma na kuwaachia waume zao jukumu la malezi ya watoto.

  Nilipotaka kujua kwanini kinababa hawa wanahofia mkakati huo wa
  kinamama walioolewa kung`ang`ania kujiendeleza kielimu, wakawa na
  haya ya kusema;
  ``Wengine ni janja yao tu, kwanini mama anayeishi Dar es Salaam,
  aende chuo cha hapa hapa halafu asirudi nyumbani akalale huko huko?

  Ukiuliza anadai eti huwa wana group discussions...kwani lazima
  majadiliano yafanyike usiku? Kwanini yasifanyike mchana, halafu
  akarudi nyumbani kwa mumewe? Mmoja aliuliza maswali yote hayo.

  Mwingine akadakiza, ``ufisadi mtupu, mama wa Dar es Salaam kulala
  chuoni na mume na wanawe wako hapa ujue ana lake jambo…lazima ana
  bwana wa pembeni huyu…``

  Mwingine akakoleza kwa kutoa mfano, ``Yuko mke wa rafiki yangu
  alipata mwanya wa kwenda kusoma ng'ambo.

  Alipomaliza masomo ya miaka miwili akatarajiwa angerudi nyumbani,
  lakini akazamia huko huko.

  ``Mume kudadisi akadokezwa kuwa mkewe alishaolewa na mzungu siku
  nyingi na wala hana mpango wa kurudi nyumbani.

  Kwa hiyo, mkakati wa kujiendeleza kimasomo kwa baadhi ya wanawake
  walioolewa, kwa kiasi fulani umelenga hujuma na usaliti kwani wengine
  wanatafutia njia ya kuondokea kama wakikuchoka``, anamalizia kusema
  baba huyu.

  Baba huyu wa mwisho alinikumbusha kisa kimoja ambapo ndoa fulani
  ilidumu kwa miaka kadhaa bila kujibu(kupata mtoto). Wakati fulani
  baba huyu akapata ajali moja mbaya ya gari.

  Chanzo cha ajali ile inasemekana alikuwa akiendesha gari huku akiwa
  anapapaswa na kidosho. Hamadi akajikuta anagonga kwa nyuma gari
  lililokuwa mbele yake na kujiingiza mvunguni.

  Baadaye akalazwa hospitalini taaban huku akiwa amevunjika sehemu
  mbalimbali za mwili. Mama akachunguza chanzo cha ajali na kupata data
  zote.

  Alichofanya ni kumuuguza mumewe hadi akapata nafuu, kisha akatafuta
  kozi yake ya nje ya nchi ambayo aliipata. Akamuacha mume huyu kwenye
  wheel-chair akihudumiwa na ndugu zake, kisha yeye huyoooo akaishia
  zake ulaya.

  Hadi leo hii inasemekana hajarejea na huko ng`ambo tayari amempata
  mzee wa kizungu ambaye anaishi naye kinyumba na wala hana mpango wa
  kurudi tena huku kwani hakuacha hata mtoto. Ama kwa hakika, Maisha
  Ndivyo Yalivyo. Au siyo msomaji wangu?

  Kwa hili unasemaje msomaji wangu? Hebu nikupe fursa nawe uchangie
  maoni tuelimishane. Hili ni tatizo linalohitaji ufumbuzi wa pamoja.
  Ukiwa tayari nikandamizie kupitia;

  Anti Flora Wingia
  Nipashe
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kuna uwezekano kuwa huyo hakuwa mke, ila alikuwa ni malaya tu au aina nyingine ya mtu. Sidhani kama hii ni kweli too fictious!
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kwa akinamama kuanzisha penzi jipya anapokuwa masomoni inategemea na mambo mengi, kuna ugumu wa kozi yenyewe, ugumu wa maisha(kama yupo nje ya nchi) marafiki na hamu binafsi.

  Nakumbuka mwaka fulani kundi kubwa la kinamama wengi wao wakiwa wameshaolewa walipata nafasi ya kwenda kusoma nje ya TZ kwa kozi ya kati ya mwaka mmoja na miwili. Wengi walikuwa katika kozi ya miaka miwili na baadhi hawakuwa na ubavu na kozi hiyo hivyo kujikuta wakitoa penzi iliwaweze kusaidiwa kufundishwa nje ya darasani.

  Wengine kipitia vipati vya hapa na pale walivyokuwa wanaviandaa,walijikuta wakianzisha mapenzi mapya na kuishia kufaidi uroda nje ya ndoa zao. Kundi hili lilikuwa na kinamama wengi zaidi na karibu kila kipati walijitahidi kuchukua kiboy kipya..!
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tusiwatukane Mama, Dada, Shangazi, Bibi zetu, kusema ukweli kufanya mapenzi nje ya ndoa hakuhitaji mke apate shule nje ya ambapo mme wake anaishi. Kama mke ni wa kufanya hayo, hata mkiwa pamoja bado anaweza kufanya.

  Kuhusu suala la mke akienda kusoma hiyo ni hatari, wakati mme akienda soma hapo si nongwa. Huo ni uwezo mdogo wa kufikiri, manake kama mme akienda nje mke akabaki, bado wote hawapo pamoja. Ni sawa tu na mke aende nje mme abaki, bado hawapo pamoja. Kama mmoja ataamua kutoka nje ni uamuzi wake mchafu ndio unamtuma.

  Likija suala la kulea watoto, kwangu mimi mke wangu akienda kusoma nitawalea, si wanangu. Kama naweza ishi na watoto wa ndugu, jamaa na marafiki, nitashindwaje mruhusu mke akasome nami nilee watoto wetu.

  Nikimalizia tu, KUISALITI NDOA HAIANGALII UKO WAPI, ni pale mtu anapoingiliwa na pepo la ngono na kuamua kusaliti. Na sio wake tu wanaosaliti ndoa, na waume pia. Suala muhimu ni kuaminiana, na kama hilo halipo kukubaliana kama mmoja anataka shule basi atafute shule ya karibu. Manake kuaminiana na kujadiliana ili upatikane muafaka ndani ya ndoa ni moja ya vitu muhimu mno.
   
 5. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2009
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nadhani ni kawaida kama wote wawili mnapendana ila inategemea pia!!
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,209
  Trophy Points: 280
  Wanaume pia wanafanya mambo kama hayo, hivyo kuelekeza lawama upande mmoja tu si haki hata kidogo.
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Akina mama wengine kama vile haitoshi uwamua kufunga pingu za maisha wakiwa huko masomoni ilhali anajua fika kuwa ameacha mume nyumbani na watoto. Muda wa kozi ubadilika na kila mwaka na kutoa ahadi kuwa anamaliza mwaka huu au ule ili kuficha ndoa yake mpya.
   
  Last edited: Mar 10, 2009
 8. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #8
  Mar 10, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mimi naona cha msingi hapa ni uaminifu tuu...hebu tuangalie na mfano uliotupa wa huyo bwana kuachwa kwenye wheelchair...kwa kweli hapo sioni kama kuna tatizo la huyo bibie kufanya hivyo na tena alitumia njia ya busara na kiubinadamu kuachana na huyo bwana bila kukorofishana. Maana tayari ndoa ilishaingia doa. Na kwa kweli wengi wa wanawake wafanyao hivyo inatokana na status ya ndoa yao, kama anaona hewa imeshachafuka basi naye ataenda kutafuta hewa safi. Hivi ngoja niulize mbona mambo kama haya yakiwatokea kina mama inakuwa issue kubwa kweli, ila ikiwatokea kina baba aaah ni haki kwao? Jamani tulio kwenye ndoa tupendane na tuheshimiane kama Mungu alivyoangiza. Hapo ndo tutakapoweza kuepukana na mambo haya yote.
   
 9. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2009
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,501
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Kwa mtizamo wangu kuna mafungu mawili ya watu wanaofanya mapenzi ndani ya ndoa (I mean wanaotoka nje ya ndoa)

  1. Kuna wale amabao wanapokuwa wanahitaji kufanya wapenzi wao wanakuwa wako mbali nao, na wanakuwa wamefikia ukomo wa uvumilivu wa kutokufanya mapenz i tena, hivyo kwa vyovyote inabidi waibe au watumie plastic toys, km zipo. Group hili lina uafadhali kidogo kwani linakuwa assumed kuwa haliwezi kutoka nje km mwenzi yuko available!

  2. Kuna wale ambao wanafanya sababu ya tamaa, kujaribu kuonja na kuchovya chovya kila mahali. Hili ni group la watu malaya na wenye tamaa kali sana ya kufanya mapenzi. Pengne labda kuna wachache wao ambao wanafanya sababu ya kutokuridhishwa na wenzi wao, lakini hii wala siyo justification ya kutembea nje sababu mwenzi anakuwa yupo available. Ni pepo la ngono tu!
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ndio maisha hayo... nakumbuka ile thread ya kusomesha mke na mafanikio yatokanayo na elimu
   
 11. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  sijui nyie watu mnaoamini kikristo sisi wa kiislamu hakuna tatizo yote sawa mume anaruhusiwa kuwa na wake zaidi ya wanne, kama kwa kila mke anakaa wiki moja hivo hadi arudi tena kwa mke wa kwanza ni mwezi mmoja, hivyo naye mwanamk anaruhusiwa kuwa na kidumu cha mkononi ingawa si lasmi
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  wacha akina mama wasome, wakiishia ujue hakua wako
   
 13. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #13
  Jan 26, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  NAUnga mguu na kipapatio hoja hii!

  Kama ni wa kumega na kumegwa atamegwa na utamega tu inakuwa kwenye damu hiyo kitu na unasubiri dirsha la upenyo wa shule kutimiza haja zako mufilisi na kitu kingine!:mad:
   
 14. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #14
  Jan 26, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Mwanamke akitaka ku-cheat anaweza kufanya hivyo mchana kweupe na jua likiwa linawaka, halafu jioni ukatoka ofisini ukampitia mkarudi wote nyumbani.

  Ni uaminifu wa mtu tu, shule isiwe kisingizio.
   
 15. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #15
  Jan 26, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  usaliti kwenye ndoa ni ulka ya mtu wapo walokwenda kusoma ndani na nje na awakusaliti ndoa zao na tuache mfumo dume huyu mtoa hoja kabezi na mfumo dume kwani si wanawake tu wanaokwenda kusoma
   
 16. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #16
  Jan 26, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Usitupotoshe
  tafadhali tuombe radhi

  Hakuna dini inayoruhusu:mad::mad::mad::mad::mad: UZINZI!
   
 17. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #17
  Jan 27, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Loh! kwa ni ruska kufanya ufuska ndani ya ndoa?
   
 18. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #18
  Jan 27, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  Kibunango, hata wanaume huwa wana tabia hiyo hiyo, mbaya zaidi, wanaume wengi wanakuwa na wanawake zaidi ya mmoja.

  Kumbuka, sisi wanaume tunaguswa kwa maumbile wakati wanawake wengi ni zaidi ya maumbile. Ndio maana ugonjwa wa mfadhaiko wa akili unawasibu Wanaume zaidi kuliko Wanawake.

  HITIMISHO:

  Both sides zinatakiwa kuwa mwaminifu.
   
Loading...