Synod
JF-Expert Member
- Oct 10, 2016
- 4,092
- 4,031
Kwanza naomba nikusahihishe, kwa mujibu wa maelezo yako, aliyetozwa hiyo faini ni mzazi na sio mwanafunzi . Ndio maana huyo mwanafunzi alirudishwa nyumbani ili kumwita mzazi wake.
Pili hapa JF hutapata jibu la uhakika, maana hiyo tozo inaaply kwenye hiyo kata uliyotaja, na sijaona mtu ana mwenye kuielewa vyema hapa zaidi ya wachangiaji wengi kuonyesha emotions zao binafsi kwa uzoefu wa maeneo mengine.
Mimi naungana na wanaohisi kuwa hiyo faini kwa mzazi imewekwa na baraza la maendeleo la kata hiyo (WDC) ambao kimsingi ndo wasimamizi wa shule hiyo. Na katika utungaji wa bylaw kama hizi, jamii (wananchi) ndo wahusika wakuu kwa maana wao ndio wanakubali au kukataa utaratibu huo kutumika. Kitendo cha kuambiwa kuwa kuna pesa taslim ambayo inabidi ipelekwe kwenye serikali ya mtaa kinaendelea kunipa imani kwamba hilo ni suala lililokubaliwa na jamii husika na utakuta hiyo pesa huko kwenye serikali ya mtaa ina maelekezo kabisa kuwa inaenda kufanya nini.
Na pengine kwa nini shuleni wanataka kupeleka ream ni kwa sababu ya maelekezo ya serikali ya kuzuia walim kukusanya michango (cash) kutoka kwenye jamii bila kuwa na kibali maalum.
Sent from my SM-T285 using JamiiForums mobile app