Mr Benja
Member
- May 28, 2018
- 44
- 40
Heshima kwenu wakuu.
Ipo hivi nina jirani yangu mwanae anasoma shule fulani hapa jijini Dar es Salaam pale eneo la Temboni-Ubungo. Ni shule ya sekondari ipo chini ya umiliki wa serikali. Wiki iliyo pita tangia tarehe 3/07/2020 mwanae (wakike) alipata ajili ya kuchubuliwa(kukatwa) na kipande cha chupa kwenye mguu wake wa kushoto na kumsababishia maumivu makali na uvimbe.
Wakati huo alikua akipatiwa matibabu ya kawaida tu ya nyumbani kwa kukanda na maji ya vuguvugu na chumvi. hadi sasa jeraha limepata auheni tunamshukuru Mungu sana hadi wakaona inafaa kumruhusu mtoto aende shule wiki hii tarehe 13 mwezi huu kwa ajili ya kuendelea na masomo.
Cha ajabu walimu wakamrudisha nyumbani ili aje na mzazi wake. Mimi pamoja na mzazi wake leo tumeenda shuleni tumesangazwa na tulio ambiwa, Ni mambo ya ajabu sana..
Eti wanasema mtoto hajahudhuria shuleni takriban wiki nzima, na kila siku moja faini yake ni Rimu moja ya karatasi nyeupe (@tsh 11000). Kwa maana hiyo mtoto hakuhudhuria siku takriban 8 hivyo ni faini ya Rimu 8 kwa ujumla wake (tsh. 88000), Pamaja na pesa taslimu shilingi elfu hamsini (50,000) kwa ajili ya kupeleka serikali ya mitaa.
Msaada wangu kutoka kwenu wajuvi wa mambo ni kutaka kujua utaratibu huu wa kutoza fani umeanza lini..? Na hatakama utaratibu huo upo je kwa mazingira ya namna hii ya mwanafunzi kupata ajali na ushahidi wa jeraha upo unamhusu vipi mtu wa namna hiyo?
Sipati picha hapa mjini ipo hivi je huko vijijini itakuwaje.