Hii imekaaje kati ya Prof. Kitilla na Magufuli

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
1,093
1,727
Kwenye hotuba aliyotoa jana mpendwa Rais wetu, kipenzi cha watanzania, kamsifia sana Prof. Kitilla Mkumbo kwa mapendekezo yake aliyotoa katika uanzishwaji wa kozi maalum ya walimu wa sayansi pale UDOM.

Lakini katika kufanya hivyo, kabainisha kuwa Prof. Kitilla ni mwanasiasa wa ACT ilihari yeye rais akiwa ni mwana CCM.

Rais akatoa wito kuwaonya wanafunzi wasijiingize kwenye mambo ya siasa. Naelewa Prof. Kitila ni mtumishi wa serikali anayefanya kazi katika taasisi ya serikali lakini ni mwana siasa. Inakuwaje rais aone ni sawa Kitilla kuwa mwanasiasa lakini afundishe wanafunzi wasioruhusiwa kuwa wanasiasa?
 
Kwenye red, sema kipenzi chako, acha sweeping statements
 
Prof Mkumbo ni kitengo angalieni sana! sana! Anafanya nini! Kibaraka wao!!
 
Haijakatazwa kwa wahadhiri kama Prof Kitila kuwa wanasiasa so long hawachanganyi majukumu yao ya kazi na majukumu ya kisiasa. Prof Kitila akiwa anafundisha hakika anaweka siasa pembeni. Na anapotumwa kuandaa mikakati kadhaa ya kufanikisha jambo fulani hakika anafanya hivyo kwa weledi mkubwa. Ndio maana Rais kamsifia
 
Rais Magufuli kamsifia sana Prof. Kitila Mkumbo kwa mapendekezo yake aliyotoa katika uanzishwaji wa kozi maalum ya walimu wa sayansi pale UDOM.

Hivi ushauri alioutoa Dr. Kitila, ulikuwa kwa niaba ya ACT Wazalendo? Kwa maoni yangu, aliutoa kama mtaalamu wa Elimu, na inawekana ALILIPWA kwa kazi hiyo. Sasa wadhifa wake wa kisiasa unaingiaje katika Hotba ya Mh. Raisi?

Napendekeza washauri wa karibu wa Mh. Raisi wamwambie tofauti za kimuktadha wa nyazifa na nafasi za watu katika Jamii. Mwalimu wangu mmoja wa Lugha alisha wahi tufundisha kwa kutoa mfano wa Mwenyekiti wa Kijiji ambaye katika Mkutano wa Kijiji watu wote (akiwemo mke wake) walim address kama Mheshimiwa Mwenyekiti.Lakini siku hiyo hiyo akiwa nyumbani, Mke wake alimkaribisha chakula kwa kusema: Baba Naonyo (Jina la Mtoto wake wa kwanza) chakula tayari. Alisema kuwa asingeweza kumkaribisha chakula kama Mheshimiwa Mwenyekiti. Na katika Mkutano wa Kijiji asingeweza kumwita Baba Naonyo.
 
Haijakatazwa kwa wahadhiri kama Prof Kitila kuwa wanasiasa so long hawachanganyi majukumu yao ya kazi na majukumu ya kisiasa. Prof Kitila akiwa anafundisha hakika anaweka siasa pembeni. Na anapotumwa kuandaa mikakati kadhaa ya kufanikisha jambo fulani hakika anafanya hivyo kwa weledi mkubwa. Ndio maana Rais kamsifia

Vilaza utawajua tu. Kwani Prof. Baregu ilikua wamfukuze mlimani ili hali wote ni wanazuoni. Au kwa vile anafanya kazi Lumumba kitila
 
Back
Top Bottom