Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 1,012
- 2,480
Bandugu, msomi mwenye degree 15 Prof. Tibaijuka amekuja na hoja ya mgombea binafsi katika chaguzi zetu. Prof amejenga hoja kwamba kulazimisha watu kujiunga na vyama vya siasa ni udikteta wa kivyama na hasa CCM kama chama tawala.
Prof anatolea mfano wa magwiji wa demokrasia duniani, Marekani. Mfumo wa kulazimisha watu kujiunga na vyama unafanya kuwaacha watu makini na mahiri wenye uwezo mkubwa wa kiuongozi na matokeo yake tunaongozwa na baadhi ya watu wajinga sana alimradi walipitishwa na vyama vyao kihalali au kiharamu.
Ifike mahali tuone ukweli kwamba kila Mtanzania anao haki ya kupiga kura na kupigiwa kura bila kujali itikadi ya vyama. Hakuna sababu ya kumuona Prof. Anna Tibaijuka kama amemwaga upupu kwenye chama chase cha CCM. Kama taifa hebu tujadiliane hoja hii ya msanifu wa jiji la Dubai na muasisi wa UN-Abitat. Tunao viongozi wengi sana nje ya vyama vyetu. Tibaijuka asishambuliwe badala yake apingwe kwa hoja si vioja.
Hata mimi natamani na nina nia ya kuwa kiongozi wa nchi lakini sikubaliani na huu udikteta na ukiritimba wa vyama. Prof. Anna Tibaijuka nakuunga mkono.
Pia soma: Kuelekea 2025 - Rais Samia, vijana tunataka tuwe viongozi, tunaomba sheria ya mgombea binafsi ili tupate nafasi kwenye vyama vya siasa, ni ngumu vijana kupenya