KASINYE
Member
- Jun 6, 2014
- 85
- 24
Binti alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mme wa mtu, penzi limenoga kiasi cha kila mmoja wao kufahamu mambo ya mwenzake kiundani, mke wa jamaa akafahamu mchezo akampandia yule dada, dada wa watu akaona imekaa vibaya akamuomba jamaa waachane asimwalibie ndoa yake, jamaa akagoma yakabaki mapenzi ya wizi.
Siku moja dada huyu akawa na shida ya fedha na mshahara haujatoka jamaa akamwambia atampa hicho kiasi cha fedha lakini aendapo safari amwachie kadi ya benki, kwavile waliaminiana hakukataa akampa kadi hiyo.
Dada amesafiri mshahara ulipotoka jamaa akatumiwa password akachukue pesa awalipe baadhi ya watu waliokuwa wakimdai dada huyu na kiasi kingine amtumie, amerudi toka safari akamweleza jamaa amepata mchumba na yeye anahitaji kutulia na mme wake.
Jamaa kuambiwa hivo akakatalia kadi ya benki demu kakomaa na msimamo wa kuachana naye na kumweleza kama kuna kitu alimnunulia kinamuuma akachukue, kweli jana jamaa kaenda kubeba TV aliyokuwa kamnunulia demu bado kadi hataki kurudisha, demu kakomaa jamaa kaenda kukomba mshahara wa dada huyu wote na masalia yake akamwamwichia 50 elfu.
Dada wa watu analia tu anatakiwa awalipie ada wadogo zake, jamaa anasema eti atamtafuta tu.
Wadau ni kwanini tusikubaliane na matokea tunapokataliwa na ukizingatia jamaa ameoa? eti hoo! tuliahidiana kuzaa naye!!!!!