Hii iliishia wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii iliishia wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Anfaal, Mar 14, 2011.

 1. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wengi wetu huenda tukawa na kumbukumbu za kutosha juu ya mafuriko yaliyotokea mkoani Kilosa mkoani Morogoro. Jitihada zilifanyika za kutosha kukusanya rasilimali na jeshi likahaamia huko kuhakikisha reli ya kati inapitika.
  Lakini pia, nchi mbalimbali zilijitokeza kutoa misaada, miongoni mwa nchi hizo Libya ilikuwepo kwenye orodha. Ahadi ya Libya ilikuwa kubwa, ya kujenga nyumba 200 kwa wananchi licha ya mahema na madawa yaliyotokea ingawa baadae CCM ilijinasibisha na ahadi ile wakati wa uchaguzi.
  Hoja yangu kubwa, je nyumba zile zilijengwa?
  Kama hazijajengwa, Libya hawakuleta ule msaada au uliletwa isipokuwa haukufikishwa mahali panapohusika?
   
 2. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  kumbuka mbagala pia...na sasa ivi gongo la mboto!!
   
 3. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Sina hakika kama nyumbazile zilijengwa maana hadi hii leo wakazi wa kilosa mafuriko bado wanalia wakihitaji misaada. Lakini hata kama libya wangetekeleza ahadi yao isingekuwa sababu ya tanzania kumuunga mkono gaddafi. Anyway misaada mingi inayotolewa tanzani haiwafikii walengwa bali inatafunwa nb wenye meno wachache.
   
Loading...