Hii ikikutokea utafanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ikikutokea utafanyaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Konakali, Aug 18, 2010.

 1. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Katikati ya mwaka 2006, ulikuwa mahali fulani ukifanya field yako ya kumalizia chuo kwa miezi sita (6) katika taasisi moja. Ukiwa completely single, ulipanga katika nyumba moja ambayo pia alikuwepo mdada mmoja naye kapanga akifanya kazi katika taasisi nyingine tofauti na ile uliopo wewe. Mdada huyu alionesha kila hali ya kukupenda na kutaka ushirikiano wako mara nyingi, kama sio zote. She is very charming to you, and very corparative. Then ukaamua kujibu hisia zake kwa namna ya kuitikia, lakini akaweka msimamo kuwa hawezi kufanya mapenzi hadi mkajitambulishe kwa wazazi, kitu ambacho kilikuwa si rahisi kwa kuwa hujamfahamu vizuri na unabanwa pia na shule yako, hata kifedha ukawa hujajipanga vya kutosha kwa hilo, kadhalika yeye mwenyewe alionesha kutokuwa tayari akidai ni mapema mno. Ila kila aina nyingine ya company uliyohitaji ulipewa. Mwanzoni mwa mwaka 2007, mdada huyo aliweza kupata kazi mkoa mwingine ambapo aliondoka na alikuaga, na akiwa huko mliendelea kuwasiliana kama miezi sita tena, ambapo alikuaga kwa simu kuwa anakwenda Ulaya kusoma. Huko mawasiliano yalipotea kabisa, na kwa kuwa pia hukupewa ahadi ya kwamba mambo yatakuaje atakaporudi, August, 2008 ulikutana na binti mwingine ambaye naye alionesha kukuhitaji katika maisha yeke, engagement ilanza baada ya muda na baadaye mkaoana June, 2009 na baada ya muda mfupi mkajaliwa mtoto. Mnamo March, 2010, ghafla uliipata "missed call", na kwa kuwa ulipata kupotezapoteza simu, namba hizi zilionekana kuwa ngeni kwako, lakini ulipiga na kuulizia "nani mwenzangu". Ukakutana na sauti yake akikujulisha kuwa amekwisharudi toka Ulaya na sasa yupo tayari kwa ulichokitaka. Msimamo wako ni kwamba haupo tayari kumkosea wala kumpoteza mkeo wa sasa. Pia usingependa kumuumiza mdada huyu, lakini ukweli wa mambo aupate. Ila tangu mlipoanza kuwasiliana tena hadi sasa hamjawahi kukutana ana kwa ana, pengine ungewezapata kumweelewesha.

  SWALI: Utafanya nini ili huyu mdada apate ukweli, tena bila kuumia wala kukulaumu, na pia bila wewe kutia doa kwenye ndoa yako?
   
 2. LeopoldByongje

  LeopoldByongje JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 373
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii Kali. Kazi kwelikweli!!!!!!!!!!!!!!! Lakini inaelekea mlizoeana na haukuwahi kumtamkia kuwa unampenda. Neno NAKUPENDA ukimtamkia mwanamke ni tunu katika maisha; na hivyo kuikana ni jambo zito kweli. Kama hivyo ndivyo; Sasa upange naye appointment kama vile ya kukutana sehemu umualike kula firigisi au nyama choma au kiti****** kutegemeana na anachopenda. Akikubali basi utakapokutana naye mpambe kweli kweli ukimpa maneno mazuri na ya laghai wakati huo ukimsoma mood yake. Iwapo utaona hajui au hana update kuhusu wewe jambo ambalo sidhani basi tumia mwanya huo umtake radhi kwa kumwambia ukweli kuhusu maisha yako; kisha agana naye kwa uungwana sana na uachane naye. Kumbuka sasa wewe ni Baba nahnhii. Kwa Mkeo uhusiano uliopo sasa ni zaidi ya mapenzi na uroda. Uhusiano wenu sasa ni maisha ya huyo mwanao na watakao fuata. Hapa ni uwajibikaji na ujenzi wa familia. Mungu akubariki katika shida hii ya Mashaka.
   
 3. JM Aristotle

  JM Aristotle Senior Member

  #3
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi kwa upande wangu bwana, hapo nadhani hakutakiwi kuwa na compromise yoyote... kwa sasa wewe ni mume wa mtu.
  Bwana, wewe mwambie ukweli kwamba umeshaoa. Usifikirie sana kuhusu kumuumiza kwasababu either way, hapo ni lazima mtu mmoja aumie. Kwahiyo jiulize mwenyewe; wa kuumia awe huyo dada au mke wako na mtoto wenu.
   
 4. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,429
  Likes Received: 1,999
  Trophy Points: 280
  mueleze ukweli kwani ukimuuma kuna tatizo gani wakati ndio ukweli wenyewe acha kum-intertain wewe tayari umeoa na una maisha mengine mwambie mapema kabisa

  Halafu unajifanya una huruma wakati huyo dada alikutosa bila mawasiliano kwa kipindi kirefu kwa nn hakuwa na mawasiliano nawe jiulize vizuri upate jibu achana na haya mambo ya ku-intertain ma-Ex wakati umeshafunga ndoa lea watoto wako na zingatia ndoa yako
   
 5. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  red: that is it... love ur wife and ur child... arrange a meeting.. you n ur spouse together with her.. Explain to her exactly hard situation u faced when she put on pending!!ASK HER WHAT SHE WOULD HAVE DONE IF SHE WORE SAME SHOES AS U DID..!!It's her loss, not urs!!:eyeroll2:
   
 6. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  mwongezee na 'chinderela' ya Ali kaiba mzee kwa kubana pua!!:smile-big:
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Mwambie ukweli kuwa umeshaoa una familia yako sasa hauko tayari kujiingiza katika mahusiano yoyote ya nje ya ndoa yako ili na yeye aangalie ustaarabu wake kwa nn alipofika Ulaya akakata mawasiliano?
   
 8. 2my

  2my JF-Expert Member

  #8
  Aug 18, 2010
  Joined: Jan 30, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo cha maana ni kumpa tu ukweli lazima itamuuma!!!!!! afu ww uendelee na familia yako!ukimuintatain sana atakuharibia ndoa yako!
   
 9. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #9
  Aug 19, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Hap mpe live tu ukiendelea kuwaza kuwa utamuumiza matokeo yake unaumia wewe sasa hata usipomwambia ukweli hauwezi kubadilika mwambie ukweli japo unauma
   
 10. RR

  RR JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Hapa mi naona opportunity...
   
 11. T

  Tall JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  1.naelewa unamtaka huyo aliekuwa ulaya na ndio maana,umetuletea hii habari.
  2.unachotaka ni tukupe mawazo ya namnagani uwe nao wawili na kila mmoja asigundue.
  3.hilo,haliwezekani kwako.baki na mkeo huyo mwingine mweleze kistaarabu kuwa........ndio hivyo tena...its too late.
  4.kwa jinsi nilivyokusoma hutaweza kasheshe za wapenzi wawili.
  5.huna haja ya kumweleza chochote mkeo,kwani kakuuliza?
   
 12. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mwambie tu ukweli kwamba hukujua msimamo wake na kwakua hamkuwa na mawasiliano uliamua kuoa, mweleze mapema ili usimpotezee muda wake
   
Loading...