Abbasfarudume
JF-Expert Member
- Feb 14, 2017
- 1,625
- 1,325
Wakuu nina maana yangu kusema hivyo, kuwa hali ya sasa hivi inatisha haswa kwenye nyumba hizi za kulala wageni al maarufu guest house ukienda sehemu sio ujichukulie tu mradi guest haswa hizi zilizo uswazi ndani ndani au za uchochoroni ni hatari sana, unashangaa katikati ya usingizi mida mibovu mnaweza kuvamiwa hata na majambazi usiku wa manane wakajua mna hela nakadhalika mkapigwa na kuteswa hata umauti unaweza mtu kukufika kisa tu ushetani na tamaa zao za mali ikichangiwa na ugumu wa maisha, sawa siwakatazi kulala guest house lkn bora mchague sehemu ilio na uhakika wa usalama na roho yako na mali zako hali imekuwa tafrani kwa usawa huu tulio nao na ukizingatia sikukuu ya eid fitri iko njiani waharifu wanatafuta hela kwa njia mbali mbali.... Napenda kuwakilisha kwenu wakuu.!