Kana-Ka-Nsungu
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 2,257
- 349
Mara nyingi najiskia kukereka ninapokutana na waswahili wenzangu ughaibuni alafu wanajidai wanaongea kiswahili kwa taabu, na most of the time kwenye mazungumzo yetu wanakuwa wakitumia kiingereza. Mke wangu sio mswahili na ninapoishi naweza kata hata wiki sijaongea kiswahili so ninapokutana na m bongo mwenzangu naona ni kama chance ya kuongea kinyumbani. Wengine ni watu niliokuwa nikiwajua toka home, tulikua tukiongea kiswahili toka enzi zile tukiwa bongo, lakini leo nikikutana nao ni mwendo wa kimombo tu! Na wengi nimewashinda kwa elimu, kiingereza nakijua lakini naona its not right kuabudu lugha ya wenzetu wakati tunaweza ku communicate kwa lugha yetu. Mbaya zaidi, wengi hawakijui kiingereza chenyewe vizuri, nikiwasikiliza tu kwenye maongezi yao nazidi kukereka kwa jinsi kilivyo broken. Je wee unaionaje hii? haijakutokea?