Hii Habari imenifanya nisikitike...

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,511
11,271
... kwa hisani ya Glopal Publishers Tz Ltd..

WASANII PIGO


Makongoro Oging’ na Rhobi Chacha
Wingu la majonzi limefunika tasnia ya filamu Bongo na kutoa pigo kuu kufuatia kifo cha kutisha cha msanii na Mkurugenzi wa Kundi la Maigizo la Jakaya Theatre linaloonesha michezo yake ITV, Thomas Senzige ‘Mr Kamati’ (29), kufariki dunia kwa kuangukiwa na kontena muda mfupi baada ya kushuka kwenye pikipiki.

Tukio hilo la kusikitisha lilijiri jioni ya Jumamosi, Mei 14 mwaka huu kando ya kituo cha daladala cha Kimara Resort, jijini Dar es Salaam.

Mbali na Mr Kamati, mtu mwingine ambaye ni dereva wa pikipiki, Renatus Aponali (25) aliyekuwa amempakiza marehemu alifariki dunia.

CHANZO CHA AJALI
Inadaiwa kuwa, lori moja la mizigo liliyumba wakati likitaka kulipita gari dogo na kusababisha kontena lililokuwa limebebwa kwenye tela kutoka na kuwaangukia watu hao ambao walifariki dunia papo hapo.


Maumivu ya kifo cha Mr Kamati yanaongezeka kwa madai kuwa, tukio hilo lilimkuta wakati ameshuka kwenye pikipiki akitokea kwenye kikao cha harusi yake, Tip Top- Manzese, Dar na kwamba, alikuwa akipokea chenji kutoka kwa dereva huyo wa pikipiki aliyemfikisha eneo hilo.

HATA WEWE UNGELIA
Haikuwa rahisi kwa mashuhuda waliokuwa jirani na tukio hilo kushindwa kuzuia machozi yao, hasa ikizingatiwa kuwa, kontena hilo lililobebwa na lori lenye namba za usajili T 840 APV kutokea Dar kwenda Morogoro lilikuwa na mzigo ndani.


Source/Chanzo cha habari

Inatosha sasa kuona kila siku maisha ya watu yanapotea kutokana na uzembe unaozuilika kabisa... JAMANI!!!
 
Jamani inauma na kusikitisha sana, poleni sana wafiwa na Mungu awape faraja ya pekee katika wakati huu mgumu!
 
Back
Top Bottom