Hii gari niliyonunua sijapigwa hapa?

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,905
44,011
Sina haja ya kueleza mengi. Mtakumbuka mwanzoni mwa mwezi huu nilikuja hapa kueleza kuwa nina nia ya kununua gari kutoka kampuni ya wauzaji SBT japani. Ni mara ya kwanza kuagiza ktk kampuno hii. Nimezoea Beforward.

Baada ya kufanya process zote za malipo na gari yangu kuaninishwa kama tayari imeshauzwa sasa nikabaki kusubir kile wanaita CAP yani Car at progress. Huu ni mfululizo wa taarifa na habari mteja hujuliwa ni lini gari inafanyiwa booking ya safari, lini itaondoka japani kuja mahali mteja alipo, meli itakayo beba na makadirio ya muda gari itawasili kwa mteja.

Baada ya kukaa siku 10 huki nikiona kimya nikawafata Sales personel huko huko. Nilichojibiwa nimeshangaa.Eti Booking inafanyika ila inakadiriwa kuanza kusafirishwa tar 29 mwezi wa tisa. Hii imenishtua. Au nililipa pesa kwa wajanja?

Kwa Beforward mamvo hayakuwa hivi. Ilichukua wiki sita tu gari zangu mbili zikanifikia. Hii ya sasa sbt wiki sita zinakatika bado haijaanza safari
 
Huduma za mwanzoni kama approval ya kupokea hela,inspection certificate umepata?. Kama tayari waulize meli gani wanategemea kutumia. Hii itakupa mwanga zaidi na kukuondolea panick. Kwa kifupi taratibu ya makampuni yako sawa. Upande wa booking inategemea vessel availability mara nyingi ni wiki 2 baada ya inspection
 
Wacha uoga hela yako Iko salama
Kila kampuni na taratibu zake
Lala usingizi
Kilichonitia woga ni huo muda mrefu. Ukiangakia from now tar 29 ni mwezi mzima na wiki moja. Hapo bado safari ya kuja huku na kushuka itachukua miezi miwili mingine.
 
Back
Top Bottom