Hii foleni mbona balaa!

​daladala zimegoma na foleni bado ndefu........mnnnnhhhhhh, kweli nchi imeendelea kwasababu ya wingi wa magari
 
Mimi kutoka MIKOCHENI mpaka Mbagala nimetumia zaidi ya masaa matano. Cha kufurahisha kuanzia k wa Azizi Ally mpaka Mtongani tulianza kutanua njia Sita mpaka upande wa pili wa barabara, yaani vurugu lililokuwepo sijawahi kuona

Kwa madereva wa dar kutanua njia mpaka kufikia sita na kuendelea sio issue kabisa. Wa mkoa ndio mana dar fujo zinawashinda, washazoea kufuata haki
 

Just a simple question to you, ni sera ipi kati ya mamia tuliyonayo inayotekelezwa kwa ufanisi? Mpaka hapo hiyo sera unayoisemea itakapotekelezwa "kiurahisi" kama usemavyo, private cars hazitokoma kamwe.
 
Haahaaa mkishafika dar mnaona kuwa mmemaliza. Mie long time kitambo nipo hapa labda nikuulize wewe unaeona usafiri wa public haufai, una miaka mingapi toka uje dar? Uliwahi ona ekarusi kumbakumba za dar enzi ya UDA legendary.

Bado sijashawishika na maneno yako. Safari ya siku 3 kwa kusimama na 15-20 yrs za maisha ya daladala za DSM hayawezi fananishwa, ila kama unawaonea gere wenye magari yao, just vaa miwani tu. Ila, watu watapaki magari yao na kupanda daladala endapo tu, hayo mnayosema ya usafiri wa umma kama Ulaya utakapoanzishwa mji huu, probably baada ya miaka 100 ijayo. Na tatizo la mji huu sio magari, tatizo ni miundombinu ya barabara. Zipo chache na nyingi ni za vumbi, wakati wa mvua kama leo, wote wanarudi kwenye lami.
 
Lakini mkuu bado ukaona priority Kwako ni smartphone baada ya kudunduliza ununue japo kwa vitz

Kaka Kariakoo kuna smartphone ya Ths 45,000 mpya ndani ya box na charger. inaitwa GALXAY asiekua na smartphone hajapenda tu. Vitz 5m sawa nitaipata kwa mkopo. tatizo petroli na sehemu ya kupaki. halafu father house akijua nimenunua gari si atanisakizia wale binti zake vicheche wasio na mpango anifumanie na mmoja anifungishe ndoa ya mkeka
 

Mkuu usifananishe vitu visivyoenda hata chembe! Unalinganisha public transport za Norway,Sweden etc na daladala za Dar?! Ushawahi kupanda daladala za mbagala au gongolamboto?! Halafu ufananishe na buses au tram za Europe.

Siku public transport yetu ikifikia hata robo ya hizo unazozisema mimi nitakuwa wa kwanza kuacha gari lakini hizi daladala nitapanda kwa shida tu ila sio kwa kupenda! Mtu anakukanyaga ukimwambia unaambiwa kakodi taxi,ukifika safari yako nguo imejikunja au kuchafuka,na inaweza hata kuchanika,umemwagiwa shombo la samaki kero kibao!
 
Watembea kwa.miguu na wenye magari ngoma droo

Kivipi? Mtembea kwa miguu jana kaloa chapachapa,mwendesha gari yuko kwenye fokeni full ac na kimziki kwa mbali! Kukiwa na foleni namna hio wala usijipe pressure,unaifuata tu. Mimi huwa natafuta tablet yangu naanza kuchat jf na kufanya mambo mengine,foleni ikisogea na wewe unasogea,sio kujipa stress utafikiri unawahi mini sijui kumbe unaenda nyumbani!
 
Mpwa Elli jiandae kesho lazima nikupige mkono na hako kagari kako ili nipate mapato....lol
Hahahahaa sijui kwanini nimechelewa kuiona hii, leo nimekaacha nimemuachia Wifi yako aendee sokoni, mie nimetembea kwa miguu ili niweze kupata "mchepuko" Lol
 
Hahahahaa sijui kwanini nimechelewa kuiona hii, leo nimekaacha nimemuachia Wifi yako aendee sokoni, mie nimetembea kwa miguu ili niweze kupata "mchepuko" Lol
"Evava",umenifurahisha sana.Mchepuko umpataye ukiwa kwa miguu ni mzuri zaidi ya umpataye ukiwa unatumia "hirizi ya mzungu".Halafu pia ni rahisi kufanya "assessment" ya ubora wa mchepuko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…