Hii foleni mbona balaa!

Hii foleni mbona balaa!

​daladala zimegoma na foleni bado ndefu........mnnnnhhhhhh, kweli nchi imeendelea kwasababu ya wingi wa magari
 
Mimi kutoka MIKOCHENI mpaka Mbagala nimetumia zaidi ya masaa matano. Cha kufurahisha kuanzia k wa Azizi Ally mpaka Mtongani tulianza kutanua njia Sita mpaka upande wa pili wa barabara, yaani vurugu lililokuwepo sijawahi kuona

Kwa madereva wa dar kutanua njia mpaka kufikia sita na kuendelea sio issue kabisa. Wa mkoa ndio mana dar fujo zinawashinda, washazoea kufuata haki
 
Lakini mbona hilo jambo ni simple, ambalo linahusu policy making pekee.

Hivi kuna tatizo gani kuintroduce mfumo ambao utazicategorize daladala kwenye classes?

Kwa mfano class X ya daladala ikawa inatoza nauli ya hivi sasa ya shilingi 600 kutoka Kimara hadi Posta, lakini ikawa haina limitation ya abiria inaowabeba.

Lakini pia ikawa introduced class Y ya daladala ambazo zitakuwa zinatoza 1,500 per trip kutoka Kimara hadi Posta, kakini daladala hizo zikapewa condition za kubeba abiriria level seat na mabasi yao yakawa na AC.

Mbona hilo linawezekana kwenye Hotel Industry?

Ukienda Serena Hotel au Kilimanjaro Hyatt, bia ile ile inayozalishwa na TBL pale Ilala ambayo 'uswazi' utainywa kwa kutozwa 2,300 lakini bia hiyo hiyo ukiingia Serena au Kilimanjaro Hotel utainywa kwa 5,000 na hakuna mtu anayelalamikia hiyo difference kubwa ya bei kwa kunywa the same brand ya bia.

Hebu watunga sera wetu waintroduce hiyo kitu kwenye Transport Industry waanze kushuhudia 'muujiza' mkubwa utakaotokea kwenye foleni jijini Dar.

Just a simple question to you, ni sera ipi kati ya mamia tuliyonayo inayotekelezwa kwa ufanisi? Mpaka hapo hiyo sera unayoisemea itakapotekelezwa "kiurahisi" kama usemavyo, private cars hazitokoma kamwe.
 
Haahaaa mkishafika dar mnaona kuwa mmemaliza. Mie long time kitambo nipo hapa labda nikuulize wewe unaeona usafiri wa public haufai, una miaka mingapi toka uje dar? Uliwahi ona ekarusi kumbakumba za dar enzi ya UDA legendary.

Bado sijashawishika na maneno yako. Safari ya siku 3 kwa kusimama na 15-20 yrs za maisha ya daladala za DSM hayawezi fananishwa, ila kama unawaonea gere wenye magari yao, just vaa miwani tu. Ila, watu watapaki magari yao na kupanda daladala endapo tu, hayo mnayosema ya usafiri wa umma kama Ulaya utakapoanzishwa mji huu, probably baada ya miaka 100 ijayo. Na tatizo la mji huu sio magari, tatizo ni miundombinu ya barabara. Zipo chache na nyingi ni za vumbi, wakati wa mvua kama leo, wote wanarudi kwenye lami.
 
Lakini mkuu bado ukaona priority Kwako ni smartphone baada ya kudunduliza ununue japo kwa vitz

Kaka Kariakoo kuna smartphone ya Ths 45,000 mpya ndani ya box na charger. inaitwa GALXAY asiekua na smartphone hajapenda tu. Vitz 5m sawa nitaipata kwa mkopo. tatizo petroli na sehemu ya kupaki. halafu father house akijua nimenunua gari si atanisakizia wale binti zake vicheche wasio na mpango anifumanie na mmoja anifungishe ndoa ya mkeka
 
It's very true, kinachotuponza sana hapa bongo ni watu kutaka kuonyesha zaidi status zao kuwa wana self drive.

Mbona kwenye nchi za wenzetu zilizoendelea sana kiuchumi, kama vile Scandinavian countries, asilimia kubwa ya wakazi wa majiji makubwa ya huko, plus wale wenye uwezo wa kumiliki magari ya bei mbaya, wanatumia Public transport za nchi hizo za mabasi na train?

Sasa hapa TZ mtu aliye nazo ukimweleza atumie public transport, ataona unataka ushushe status yake, wakati bila kujua kwa kuwa hizo private cars ndiyo zinazokuwa zimefurika mabarabarani, ambazo most of the time unakuta kwenye gari nzima yumo yeye peke yake anayedrive gari hiyo, unakuta anapoteza masaa kadhaa humo barabarani.

Ni vyema kama waTZ tutakuwa na nia ya dhati ya kuondoa traffic jam hapa jijini Dar, itabidi na mindset zetu ni lazima zibadilike, za kujua kuwa the only permanent solution za foleni za mabarabarani ni kuimarisha public transport na wakazi wa jiji hili waprefer kutumia public transport badala ya private cars zao.

Kama fikra hizo hazitabadilika vichwani mwetu, hata huo mradi wa BRT utakapoanza, hautaleta muarobaini wowote na bado adha ya foleni ya magari itakuwa haijawa solved hata kidogo.

Mkuu usifananishe vitu visivyoenda hata chembe! Unalinganisha public transport za Norway,Sweden etc na daladala za Dar?! Ushawahi kupanda daladala za mbagala au gongolamboto?! Halafu ufananishe na buses au tram za Europe.

Siku public transport yetu ikifikia hata robo ya hizo unazozisema mimi nitakuwa wa kwanza kuacha gari lakini hizi daladala nitapanda kwa shida tu ila sio kwa kupenda! Mtu anakukanyaga ukimwambia unaambiwa kakodi taxi,ukifika safari yako nguo imejikunja au kuchafuka,na inaweza hata kuchanika,umemwagiwa shombo la samaki kero kibao!
 
Watembea kwa.miguu na wenye magari ngoma droo

Kivipi? Mtembea kwa miguu jana kaloa chapachapa,mwendesha gari yuko kwenye fokeni full ac na kimziki kwa mbali! Kukiwa na foleni namna hio wala usijipe pressure,unaifuata tu. Mimi huwa natafuta tablet yangu naanza kuchat jf na kufanya mambo mengine,foleni ikisogea na wewe unasogea,sio kujipa stress utafikiri unawahi mini sijui kumbe unaenda nyumbani!
 
Mpwa Elli jiandae kesho lazima nikupige mkono na hako kagari kako ili nipate mapato....lol
Hahahahaa sijui kwanini nimechelewa kuiona hii, leo nimekaacha nimemuachia Wifi yako aendee sokoni, mie nimetembea kwa miguu ili niweze kupata "mchepuko" Lol
 
Hahahahaa sijui kwanini nimechelewa kuiona hii, leo nimekaacha nimemuachia Wifi yako aendee sokoni, mie nimetembea kwa miguu ili niweze kupata "mchepuko" Lol
"Evava",umenifurahisha sana.Mchepuko umpataye ukiwa kwa miguu ni mzuri zaidi ya umpataye ukiwa unatumia "hirizi ya mzungu".Halafu pia ni rahisi kufanya "assessment" ya ubora wa mchepuko.
 
Back
Top Bottom