mkolosai
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 1,578
- 1,104
Wadau ukifika Dodoma Kabla hujaingia mjini kuna ghorofa la Kilimo kwanza huwa wanauza matrekta, naombeni kujuzwa kuhusu hii fence mmiliki wake ni nani maana ipo ndani ya hifadhi ya barabara. Bikoni zote mbili zinaonyesha jamaa wamevamia barabara.
Awali hii fence ilikuwa ya tofari na iliwekewa alama ya X na maneno kuwa BOMOA. Baadae ikapigwa rangi nyeupe ili kufuta yale maneno. Siku zilivyoenda ikavunjwa na kubadilishwa kuwa fence ya nondo ambayo hata ukiandika neno Bomoa halionekani. Sasa swali mheshimiwa Rais ama watendaji wako hawaioni hii fence kuwa ipo ndani ya hifadhi ya barabara?
Na je ina maana kuna mtu yeyote yupo juu ya maagizo yako mheshimiwa Rais ama hata sheria za nchi kuwa ujenzi ndani ya hifadhi za barabara ni marufuku? Nawasilisha