Ngho
Senior Member
- Jun 2, 2015
- 121
- 189
Kwanza niipongeze serikali kwa kuanzisha elimu bure, kwani imekuwa chachu na hamasa kwa wazazi kuona kama gharama zinapungua kwa kumsomesha katika mfumo huu wa elimu bure. Jambo ambalo sio sahihi.
Hii elimu bure ni changamoto kwa walimu hata wazazi, na imeshindwa ku-guarantee ubora wa elimu yetu kwa sababu zifuatazo.
Mosi, gharama za uendeshaji shule na kiasi cha pesa kinachotolewa kutoka serikalini hakitoshelezi mahitaji ya shule husika, kwa mfano shule x inaweza kuwa inapokea 1.2mil. ambayo ndani yake kuna posho ya madaraka, pesa ya stationary, vifaa vya michezo, dawa (first aid), ukarabati, mlinzi, na vibarua wengine. HII pesa huwa haitoshi, wakuu wa Shule wameshindwa kulalamika wanaendelea na uvumilivu USIO na tija.
Pili, elimu bure imewalazimisha wazazi wawe wachangiaji wa mara kwa mara kuokoa jahazi, mfano mzazi anaweza kufikisha hata 150k, ambapo before elimu bure mzazi alikuwa analipa almost elfu 40 a year.
Tatu, wanafunzi wamekuwa wanakosa miundombinu mizuri ya kujifunzia ikiwa uwepo wa SAMANI za kutosha kwa kuwa serikali haijihusishi sana katika kuangalia ubora wanaouhubiri.
KUTOKANA na hoja hizo serikali inapaswa kuliangalia ili kuboresha kwa ufanisi mpango uliokusudiwa. FREE AND BETTER EDUCATION, na sio FREE AND BITTER EDUCATION.
Mwisho serikali inaweza kuamua, kati ya kuboresha ili ufanisi na ubora wa elimu inayotolewa mbele ya changamoto tajwa hapo juu au irejeshe mfumo wa kulipia kama zamani.
NAWASILISHA