Hii Clip imfikie Rais Samia, ukweli mchungu ambao waliomzunguka hawataki ausikie

Hilo ni moja Kati ya mambo mazuri ya Nyerere na kuna mengi mazuri ya JPM simple

Siangalii mazuri boss, naangalia wajibu kwakuwa kiongozi analipwa mshahara. We ndio unaangalia kwa mtazamo wa mazuri. Hata hivyo hoja hapa haikuwa mazuri ya kiongozi fulani, bali we kutaka kuonyesha Magufuli alikuwa bora kwenye maamuzi ya mambo haya. Nimekuwekea mifano halisi kuwa msipotoshe maana haya kuwa hata kwenye utawala wa Magufuli yalikuwa ni haya haya.
 
Pmj na katiba ya Kenya ila ufisadi Kenya Ni wa kutisha mno Ni taifa la kwanza africa mashariki na Kati kwa ufisadi katiba Yao iko vip
Tunaona ufisadi wa Kenya vizuri maana kuna uhuru wa vyombo vya habari kuliko hapa. Uhuru wa habari hapa ungekuwa kama Wakenya, huenda tungeongea hadithi tofauti
 
oi mzee me sijasema jinsia ndo ina-matter pekee nilichokisema ni kwamba nchi inahitaji kiongozi strong na asie na woga kama Hayati ili tuone mabadiliko ya hali mbaya iliyo sasa
Nani muoga Sasa? Na anamuogopa Nani?

Pili Mwendazake alikuwa strong sawa how comes ufisadi ukitamalaki awamu ya 5?

Mabasiliko yapi unadhani Mwendazake angefanya zaidi ya kuwaambia hajaleta ukame na vita ya Ukraine?

Kwani wakati mnalalamika njaa aliwaaambia yeye ndio aje awalimie?

Wakati mnalalamika maisha magumu/vyuma kukaza aliwajibuje?

Wakati mnalalamika tetemeko aliwajibuje? Alileta suluhu?
 
FB_IMG_1667288639541.jpg
 
Nimesikiliza kwa kiasi ila huyo mwanamama nimemdharau kwa sababu zifuatazo..

Kwanza Eti ooh Tanzania haikuwa tayari kwa Rais Mwanamke na blaa blaa kibao,huu Ni ujinga na upuuzi..

Pili,Eti pili Rais anasafiri sana,hivi hii Ni hoja? Rais kusafiri na kutosafiri ndio Nini? Kusafiri makes sense na Hadi sasa imemake sense..

Alete namba Basi tulinganishe Mwendazake ambae hakusagfiri na Samia ambae amesafiria tuone impacts..

Mwisho Ni lini Tanzania haikuwahi kuibiwa kabla ya Samia? Kuibiwa kunahusianaje na jinsia ya mtu?

Hilo limwanamke linaongea Liko Marekani kwa Nini lisije kuishi Bongo ili kufanya justification ya linachoongea?
Njaa zinakuondolea dignity
 
Hapana kwa Kenya uliona Kenyatta alibwagwa bungeni pale alipotaka kukopa zaidi.... Pia mahakama ilizuia mambo kadhaa mfano BBI referendum ambayo Inge cost mabilioni, ikazuia manunuzi kadhaa ya serikali mfano mradi wa consolidated ID cards n.k tuliona magovernor mfano Sonko na Waititu wakiwa impeached kwa ufisadi!! Hayo bongo haiwezekani maana mahakama inateuliwa na Rais so inakua ngumu kumnyoosha bosi wako!!

So suluhisho ni katiba sio uongozi Wala chama..... The more independent bodies we have the more accountable the government gets.
Ndiyo, niliyaona hayo ya BBI na mengine, na niliyaona pia ya mikataba ya SGR pamoja na mahakama kuamru iwekwe wazi, lakini haikuonekana popote hadi juzi, kumbe alikuwa anasita kuiweka wazi kwa vile waKenya wenyewe ndio walioruhusu upigaji mkubwa katika mikataba hiyo.
So suluhisho ni katiba sio uongozi Wala chama..... The more independent bodies we have the more accountable the government gets.
Hapa naona tutarudi kule kule kwa jana, kwa sababu tofauti zetu ni kubwa sana juu ya hili.

Nakubali kabisa umuhimu wa kuwepo na Katiba inayosimamia yote yaendeleayo ndani ya nchi, lakini uwepo wa katiba pekee hautoshi kabisa, bila kuwepo na watu wanaoiheshimu na kuitekeleza hiyo katiba na sheria zinazotokana nayo.
Hawa watu ndio viongozi wa nchi, ambao nao wanaongozwa na msimamo wa chama chao.

Hii mihimili inayoainishwa kwenye katiba, ufanisi wake wa kufanya kazi nao unategemea na watu wanaoisimamia mihimili hiyo.
 
Tunaona ufisadi wa Kenya vizuri maana kuna uhuru wa vyombo vya habari kuliko hapa. Uhuru wa habari hapa ungekuwa kama Wakenya, huenda tungeongea hadithi tofauti
Hata Sasa Uhuru upo ndio maana mnapayuka ,kipindi Cha Mwendazake mliufyata wala hamkuweza hata kupost picha za watoto wenu waliorundikana kwenye vyumba vya madarasa wakikaa chini..
 
Siangalii mazuri boss, naangalia wajibu kwakuwa kiongozi analipwa mshahara. We ndio unaangalia kwa mtazamo wa mazuri. Hata hivyo hoja hapa haikuwa mazuri ya kiongozi fulani, bali we kutaka kuonyesha Magufuli alikuwa bora kwenye maamuzi ya mambo haya. Nimekuwekea mifano halisi kuwa msipotoshe maana haya kuwa hata kwenye utawala wa Magufuli yalikuwa ni haya haya.

Ingekuwa tunaweka Kwa asilimia then tungesema JPM ana 90% ya kujali uwajibikaji
 
Sasa kaka kama tume ya uchaguzi ipo chini ya sisiem kuna upinzani atakayelamba asali. sasa cha kuwasahaulisha watanzania wajinga ni pale uchaguzi unapokaribia bas atafanya mambo mazuri mawili matatu watu watasahau shida zote watashuka wino shwaaaah
 
Nimesikiliza kwa kiasi ila huyo mwanamama nimemdharau kwa sababu zifuatazo..

Kwanza Eti ooh Tanzania haikuwa tayari kwa Rais Mwanamke na blaa blaa kibao,huu Ni ujinga na upuuzi..

Pili,Eti pili Rais anasafiri sana,hivi hii Ni hoja? Rais kusafiri na kutosafiri ndio Nini? Kusafiri makes sense na Hadi sasa imemake sense..

Alete namba Basi tulinganishe Mwendazake ambae hakusagfiri na Samia ambae amesafiria tuone impacts..

Mwisho Ni lini Tanzania haikuwahi kuibiwa kabla ya Samia? Kuibiwa kunahusianaje na jinsia ya mtu?

Hilo limwanamke linaongea Liko Marekani kwa Nini lisije kuishi Bongo ili kufanya justification ya linachoongea?
Aise akili yako ndogo mithili ya pilitoni. Na haupaswi kuwa jamii forum.
 
Na wewe mtoa mada nirudi kwenye mchango wako,Kipi hasa Cha Maana ambacho Magufuli alifanya kikakufaidisha wewe binafsi achilia mbali blaa blaa zingine?

Maana katika Rais wa hivyo Ni Magufuli alikuwa failure kwenye Kila kitu kuanzia Uchumi Hadi huduma za jamii..

Swala la maisha ya Mtaani kuwa Magumu kwani hujui Ni global issue?

Labda nikuulize Vyuma kukaza ilikuwa inatamkwa wakati gani? Watu kufungua biashara na kukimbia ilikuwa Ni awamu gani? Vipi saizi hizo lights zinasikika? Unasikia watu wakilalamika kuporwa Pesa na TRA au kufungua biashara?

Umesikia ajira hazitoki Kama awamu ile iliyokuwa imeshindwa kuleta Mambo sawa na kusingizia mabeberu na excuses zingine za kujenga bwawa,reli na blaa blaa kibao?

Kinachoonekana hapa Ni shida za kisaikolojia na mfumo dume nothing else..

Mwisho Mimi ukiniambia nifanye rating naona Rais Samia ndio amefanya vizuri zaidi kuliko Marais wote niliowahi kuona wanaongoza..ukitaka sababu nitakueleza.
We jamaa baada ya mpango wako na yule mhaya bashiru kubuma akili bado hazijakukaa sawa, Naona Kama una hangover vile
 
Sawa Cha Maana alichoongea huyo mwanamke wa Ulaya Ni kipinhasa wewe umetoka nacho?
Udhaifu wa kiongozi wetu mkuu katika uongozi wa nchi.

Sikubaliani na huyo mama mwenye sauti katika mambo kadhaa, moja ikiwa ni kuhusisha jinsia ya kiongozi wetu kwa hali isiyoridhisha. Nadhani hata yeye kaliongelea tu bila ya kulipa tafakari jambo hilo.
 
Thibitisha huo udhaifu na sisi tuuone
 
Back
Top Bottom