Mimi ni Tomaso, hiki kigeu geu cha ghafla kinanitia wasiwasi, juzi alikuwa na wauaji leo anawatetea aliowasaliti juzi, je ni dhamiri yake au kuna msukumo wa nje au kuna project ambayo watawala wanataka waifanye kwa kutumia mgongo wake baada ya kushindwa kumshawishi Warioba.
Ni juzi tu alikuwa akiwananga vijana kuwa watoe hoja kwa utaratibu si maandamano, akawaambia hoja hazitatuliwi kwa kuharibu mali, ni juzi tu alisikika akimwambia Kapteni Tesha aliyewatetea vijana kuwa sio askari hana nidhamu ni muhuni.
Leo anawaambia vijana wana haki ya kuandamana, anawaambia watawala kuwa wasiseme hawawajui wauaji, anamwambia Katibu Mwenezi CCM kuwa anafanya siasa za hovyo, anawaambia CCM kuwa wanafanya siasa huku CHADEMA na mkiti wao LISSU wamewafungia kufanya siasa.
Wasiwasi ndio akili, ngoja niendelee kuwa tomaso hadi trh 22/1 atakapokutana na wazee wa Dar kina Kikwete labda nitaelewa lengo lake hasa ni nini.