ruaharuaha
JF-Expert Member
- Feb 14, 2018
- 4,452
- 5,670
Mpango mzima ni kwamba hiyo tarehe 22/01/2026, hao wazee watakaa na kutoka na kauli kwamba Lisu aachiwe, chadema ifunguliwe, Mchakato wa katiba na Tume Huru uanze na au uharakishwe ili kuondoa malalamiko ya wananchi.
Hawa wazee ni kama vile wanatuona hatujui ni mchezo gani wanataka au wapenga kuufamya.
Halafu serikali itatekeleza maazimio yao na kusema kwamba imewasikiliza wazee wenye Busara na ndicho ilicho kifanya- just to save face.
Haya mambo ya kesi ya Lissu na kufungukiwa kwa wapinzani- Lissu na Mpina, hayakutakiwa kabisa kutokea kabisa...
Cha ajabu hawatasema chochote kuhusu kuwaondoa, kuwashitaki, kuwawajibisha wale wote waliosababisha, kupanga na kutekeleza maovu,utekaji, ufiraji, utesaji, mauaji ya wananchi wakianza na genge la Samia kama chanzo cha machafuko yote haya.