Hifadhi yatoa ofa ya mende siku ya Valentine

Hifadhi yatoa ofa ya mende siku ya Valentine

majoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Posts
2,762
Reaction score
5,363
Nailete kama nilivyoikuta. Wale wapendanao wa JF mnasemaje.... na sisi tuanzishe la kwetu humu

Hifadhi yatoa ofa ya mende siku ya Valentine kwa wapenzi walioachana (EX)
Hifadhi yatoa ofa ya mende siku ya Valentine kwa wapenzi walioachana (EX)





Maafisa wa kituo cha maonesho ya wanyama cha San Antonio nchini Marekani wametoa ofa kwa mwenye Dola 5 sawa na Sh. 11,550, atapewa Mende ampatie jina la mpenzi wake wa zamani (Ex) na kisha kumlisha mnyama yoyote kwenye siku ya wapendanao ‘Valentine Day’.



Valentine1.jpg


Mende na Ua la Valentine
Tukio hilo limepewa jina la “Cry Me a Cockroach” ikimaanisha ‘ning’ate mimi Mende’ ambapo wataruhusiwa hata wale ambao wapenzi wao wa zamani hawaishi Jijini Texas na Marekani kwa ujumla.
💔We're hosting the first-ever “Cry Me a Cockroach” event. You can name a live cockroach, and we'll serve it up as a snack to one of our animals. You could even name a rat, and we'll feed it to a reptile!
🐀🐍
kywVRVr1

Cry Me A Cockroach | San Antonio Zoo
Broken Hearted This Valentine’s Day? Purchase A Cockroach Or Rat, Name It After Your Ex, And We’ll Feed Them To One Of Our Animals
Kwa wale ambao wapenzi wao wa zamani walikuwa ni wabaya zaidi kwao au wakatili, watatakiwa kulipia Dola 20 sawa na Sh. 46,206 ili kupewa panya na kuwapa majina ya wapenzi wao wa zamani kisha kuwalisha wanyama.
Hiyo itakuwa ni kwa mara ya kwanza kwa kituo hicho kufanya tukio la aina hiyo ambalo limezua hisia za mshangao na kuvutia kwa watu mbalimbali.
By Ally Juma.
 
Fikra za haraka zikanituma labda kwa heshima ya style pendwa ya kifo chake.
 
Fikra za haraka zikanituma labda kwa heshima ya style pendwa ya kifo chake.
Ha ha haaaaa inawezakana kuna kiunganishi cha staili ya mende na kumpa jina la x mende
 
Wamewaza vyema, kila atakayeenda kumnunua mende na kumpa jina la mpenziwe wa zamani ni lazima yuko bitter, kwa kufanya hivyo atapata relief na pengine akapona maumivu ya mapenzi aliyosababishiwa.
 
Niko kijiji cha nkasi ila kwanzia tareh 13 ntakuwa dar kuikaribisha Valentine na mifugo yangu unanua ka panya nambandika karatasi tunaandika jina la yule ex wako namuweka kwenye cage ya mifugo yangu (nyoka) hii biashara nimeipenda naja nayo huko hawa nyoka nawafuga kama pambo sikujua baadhi ya application zake ukiachana na kuwafungulia wawagonge adui zangu Leo mtoa mada umenipa ubunifu karibuni

Kama ulimpa nauli akala hakutokea karibu pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom