Hifadhi ya Serengeti yatwaa tuzo ya Ubora Afrika

Kuna maswali ya kujiuliza hapa, ni nani alishinda kabla kwenye tuzo za awali za World Travel, na pia tuzo za mwaka huu za Safaribooking na za kabla ya mwaka jana, ni akina nani walikuwa wanapata tuzo hizi? Tufanye consistency analysis na pia factors contubuting to award. Hii inaweza kutufanya tuwe na mikakati imara kuliko kushangilia hii half and biased infomation.
 
Hifadhi ya Taifa Serengeti imeshinda tuzo ya kuwa hifadhi bora kwa Bara la Afrika kwa mwaka 2019, tuzo iliyotolewa jana na Taasisi ya World Travel huko nchini Mariutius.

Hii ni ya pili kwa Hifadhi hiyo ya Serengeti kutangazwa kuwa hifadhi bora Afrika baada ya mwaka jana 2018 kushinda tuzo hizo kupitia mtandao maarufu wa safari za utalii dunia wa safaribooking.com.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, washindi katika tuzo hizo za WTA hupigiwa kura na wabobezi katika masuala ya safari na utalii duniani kote.

Wengine walioingia katika kuwania tuzo hizo ni pamoja na Hifadhi za Taifa za Central Kalahari ya nchini Botswana, Hifadhi ya Taifa ya Etosha ya nchini Namibia, Hifadhi ya Taifa ya Bonde la Kidepo Uganda, Hifadhi ya Taifa ya Kruger nchini Afrika kusini na Hifadhi ya Taifa ya Masai Mara ya Kenya.
Inatusaidiaje?
 
Vipi kuhusu Wakazi wa hiyo Hifadhi na Wao wametajwa kuwa katika Maisha bora ya Kiwango gani duniani yaliyotokana na kuwa karibu nayo?
Wakazi wa hifadhi hipi? Hifadhini wanaishi wanyama... Weka swali lako vizuri... Serengeti hakuna makazi ya watu... Ni wanyama pori tuu.
 
Habari njema hii, nashauri Tanapa wangetoa video fupi ya serengeti dk 1, kwa lugha ya biashara,wanyama na madhari. Hizo barua rasmi tunasoma kichwa cha habari wachache tu hapa Tz.Ila video amazing itaruka dunia nzima.
 
NI KWELI KABISA
 
Vipi kuhusu Wakazi wa hiyo Hifadhi na Wao wametajwa kuwa katika Maisha bora ya Kiwango gani duniani yaliyotokana na kuwa karibu nayo?
Nimeshatembea sna huu mkoa wa mara hasa wilaya ya serengeti

Nahis miongoni mwa wa watanzania wanaoishi maisha duni kabisa basi ni wao

Vijumba ni vyasi tupu daah
 
Back
Top Bottom