Hichi ni kizazi cha udsmi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hichi ni kizazi cha udsmi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Jul 18, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jul 18, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  HICHI NI KIZAZI CHA UDSM

  Sasa imetimia zaidi ya 12 toka kuanzishwa vyama vingi nchini Tanzania , kuanzishwa kwa vyama hivi ilionekana kama vile ndio mwokozi Fulani hivi kwa wananchi wa Tanzania ambao walikuwa wanahitaji mabadiliko katika sehemu mbali mbali za jamii zao

  Katika uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi , vyama vya upinzani vilikuwa na nguvu kidogo kuweza kusema sera zao na kukubalika hata mgombea wa upinzani wakati huo aliweza kueleweka kwa wananchi kwa kiasi kikubwa hivyo hivyo kwa uchaguzi wa mara ya pili .

  Inajulikana kilichotokea Zanzibar , baada ya watu kadhaa kuuwawa na kuumizwa katika uchaguzi huo katika harakati zao za kudai matokeo ya haki ya viongozi waliowachagua wao

  Uchaguzi wa mara ya tatu ari imeonekana kushuka sana , baada ya kilichoonyeshwa Zanzibar huo ubabe na utumiaji wengine wa nguvu kulazimisha matokeo au kununua shahada pamoja na njama zingine zilizo kinyume cha sheria

  Kuanzia wakati huo sasa ndio tu tumeanza kuona watu wakihama vyama toka kimoja kwenda kingine kwa ajili ya maslahi zaidi ya mambo yao binafsi wengine walirudi chama tawala na kupewa vyeo vikubwa serikalini au katika chama tawala .

  Hii kuhama hama vyama ndio kumetengeneza mamluki wengi sana mpaka sasa hivi ambao wengi wako katika vyama vya upinzani , mfano mzuri upo wakati wa uchaguzi wa mbeya vijijini baadhi ya watu walivyopandikizwa katika vyama vya upinzani .

  Kwa kuwa watanzania wengi walitegemea sana upinzani kwa ajili ya kutoa vilio vyao pamoja na kero zao zingine kwa sasa hivi , upinzani huu unaonekana umepwaya kwa namna moja haswa kutokana na matokeo ya chaguzi 2 zilizopita mwaka huu pekee .

  Wapinzani hawaaminiki tena , unaweza kukuta wapinzani hao ni mamluki , unachopeleka ndio kinaweza kutumiwa dhidi yako huko mbeleni , watu wanaogopa kufanya mabadiliko ya kweli katika jamii zao kuogopa kupoteza nafasi Fulani katika jamii hizo hizo wanazoziongoza .

  Hata hii vita dhidi ya ufisadi ambayo kwa kiasi kikubwa imechochewa na wapinzani kwa sasa inaonekana kukosa nguvu na mwelekeo baada ya baadhi ya wapinzani kukubali kutumika kwa ajili ya maslahi ya watu wachache yaani kukubali kunyamazishwa kwa njia mbali mbali , labda kuingizwa kwenye kamati zinazowabana au shuguli zingine ambazo zinawafanya wasiweze kuongea na kusikika kwa sana .

  Kwa kuwa wapinzani wameshindwa kuonyesha njia na nia njema ya kukomboa taifa hili ambalo liko katika hali mbaya sasa hivi , basi ni wajibu kwa kila mtanzania haswa kijana atambue sasa anatakiwa wewe popote alipo alete mabadiliko yake mwenyewe pamoja na ya watu wanazunguka eneo hilo watakuwa kidogo kidogo kwenda kimataifa .

  Ni wakati sasa watanzania tupiganie haki zetu za msingi kama nchi sio Juu OIC ambayo ni kundi la watu wachache , au Mahakama za Kadhi na makundi mengine ambayo yanafanya wananchi watengane huku mafisadi na wafilisi wengine wa nchi wakiendelea kutufilisi sisi na vizazi vyetu .

  Hawa viongozi wa sasa karibu wote ni wasomi wa ndani , wamesoma katika chuo kikuu cha daresalaam na wengine hata wamewahi kuwa walimu katika chuo hicho na vyuo vingine hapa nchini , wengi hawa enzi za mwalimu walisomeshwa bure kabisa .

  Viongozi wanachofanya kwanza ni kudhalilisha wanataaluma wote waliowahi kupita katika chuo cha UDSM na Tanzania kwa ujumla , hamna wakati ambao chuo kimoja kimepata kutoa viongozi wan chi wengi kama uongozi wa wakati huu kuanzia raisi wan chi ,baadhi ya mawaziri , wabunge , makatibu wakuu na wafanyakazi wengine walio katika sekta zingine nyeti

  Pia hakuna wakati ambapo nchi imewahi kuwa na matatizo kama sasa hivi ambapo viongozi hawa ndio walitakiwa kuwa mfano kwa kuwa bora zaidi hili ni zao la ha hapa nchini kwanini wanafanya hivi ?
   
Loading...