Kwanza, nilichotaka kusema ni kutoa hoja ya kuomba shughuli za Bunge zisitishwe kwa muda ili Kamati ya Uongozi ya Bunge ijadili makandokando yote ambayo yalikuwa yametokea juu ya muswada huo, ukiwamo uongo wa mwenyekiti wa kamati ya Bunge, uongo wa serikali bungeni na masuala mengine yote, ili sasa Bunge lipate mwelekeo chanya juu ya muswada huo na mchakato mzima wa Katiba Mpya kwa masilahi ya wananchi.
Hivyo hoja yangu ilikuwa muhimu sana kusikilizwa, ili viongozi wakutane kuokoa jahazi na kuondoa sintofahamu ambayo hatimaye imesababisha mjadala mkubwa na muswada mbovu kupitishwa bungeni kwa masilahi ya upande mmoja wa CCM, Mbowe alikaririwa akisema.