Hiace ipi inafaa kwa daladala kati ya 2000cc au 3000cc?

JMF

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
1,758
2,769
Salaam wakuu.
Nina mpango wa kununua Toyota HiAce kwaajili ya kufanya kazi kama daladala. Kuna kitu nimeshindwa kuelewa kama nichague yenye engine ya 2000 au 3000. Pia kuna option ya manual au automatic. Na pia diesel au Petrol. Naombeni msaada kwa wenye uzoefu katika magari wakuu.
 
Petrol ni nzuri kwenye milima mikali.
2000 ni nzuri kwa tambarare na iwe Diesel
Manual yafaa kwa daladala
 
  • Thanks
Reactions: JMF
Asanteni kwa ushauri wenu maana nimepata mwanga. Nahitaji iwe na nguvu ya kutosha ili hata kwenye milima ipande bila tabu ikiwa na abiria. Naona automatic haifaii wala petrol haifai. Issue ipo hapo kwenye engine Eminentia, nzalendo
 
Usithubutu kununua Hiace ya Petrol. Hakikisha engine inakuwa ya diesel. Ikiwa manual ni poa zaidi, but auto sio mbaya pia... NB Sidhani kama kuna engine ya diesel ya cc 2000. Ukiona hivyo ujue hiyo ni ya Petrol. Engine ikiwa ya Diesel ikawa ya cc 2400 hiyo gari lazima itakuwa na Turbo... So standard kwa Hiace nyingi ni kuanzia cc 2700 kwa engine ya Diesel.
 
Back
Top Bottom