Sitazungumzia kodi ya TRA, Service Levy ni kodi ya Manispaa ni sawa na ile ya Maendeleo, kodi hii IPO kisheria isipokuwa walizembea kuidai kwa miaka mingi na sasa imekumbukwa. Tatizo pekee lililopo ni kwa baadhi ya wafanyabiashara kutozwa kodi hii mara mbili na hawa ni wale waliopo kwenye masoko ambapo Jiji hukusanya Service Levy sh.1,000/= kila siku mwaka mzima na ukienda kuchukua leseni ya biashara unalipishwa tena! Ni juu ya wafanyabiashara hao kusimama na kusema hapana vinginevyo Manispaa utailipa sh1,000× mwezi mmoja × miezi 12 + sh.81,000/= na Manispaa itajitapa imevunja rekodi kwenye makusanyo ya kodi, Alhamdulilah mwenye kupata kapata.