Hezbollah:Hakuna hata sehemu moja ndani ya Israel ambayo itasalimika na makombora yetu

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,890
Hizbullah: Hakuna hata sehemu moja ya Israel itakayosalimika na makombora yetu
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, hakuna hata sehemu moja ya Israel ambayo haiwezi kufikiwa na makombora ya harakati hiyo ya muqawama.
Sheikh Naim Qassem ameyasema hayo katika mahojiano na gazeti la al-Vefagh linalochapishwa mjini Tehran na kufafanua kuwa: "Hakuna hata sehemu moja ndani ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu isiyoweza kufikiwa na makombora ya Hizbullah."
Utawala wa Kizayuni wa Israel umeshawahi kufanya uvamizi na hujuma kadhaa za kijeshi katika mpaka wake wa pamoja na Lebanon, na hivi karibuni waziri mmoja wa utawala huo ghasibu alidokeza kuhusu uwezekano wa kuivamia tena Lebanon kwa lengo la kubomoa kile alichodai kuwa ni njia za chini kwa chini zilizochimbwa na Hizbullah.
Kuhusiana na vitisho hivyo, Sheikh Naim Qassem amesema: "Wazayuni hawawezi kuhimili hatari kubwa kama hiyo kwa kutaka kupambana na Hizbullah, na ndiyo maana hawana mori wa kuingia katika vita vingine na Lebanon."
Ameongeza kuwa, harakati hiyo ya muqawama ya Lebanon imejizatiti kwa kinga ya ulinzi ambayo imeifanya Israel isithubutu kuanzisha chokochoko dhidi ya Lebanon tangu baada ya vita vya mwaka 2006.
"Hata wanapotoa vitisho huwa wanasema, 'ikiwa Hizbullah itatushambulia' tutajibu mapigo, kwa sababu mikakati iliyowekwa na Hizbullah ndani ya Lebaon imeifanya Israel iiwiye vigumu mno hata kujiwa na wazo la kuanzisha vita dhidi ya Lebanon", amesisitiza Sheikh Naim Qassem.
Wiki iliyopita utawala wa Kizayuni wa Israel ulianzisha kile ulichokipa jina la "Operesheni ya Ngao ya Kaskazini" ya eti kufichua na kubomoa njia za chini kwa chini zilizochimbwa na Hizbullah kuelekea ndani ya Israel.
Waziri wa Intelijensia na Usafiri wa utawala huo Yisrael Katz alitamka siku ya Ijumaa kwamba, huenda ikahitajika vikosi vya jeshi la Israel viingie ndani ya ardhi ya Lebanon kwa ajili ya kuzishughulikia njia hizo.
Endapo utawala wa Kizayuni wa Israel utaanzisha uchokozi na uvamizi dhidi ya Lebanon utaibua moto mkali wa makabiliano makali kati yake na Hizbullah.
Harakati hiyo ya nchini Lebanon imeshaonya kuwa utawala huo haramu "utajuta" endapo utaivamia nchi hiyo.../
 
Waziri wa Intelijensia na Usafiri wa utawala huo Yisrael Katz alitamka siku ya Ijumaa kwamba, huenda ikahitajika vikosi vya jeshi la Israel viingie ndani ya ardhi ya Lebanon kwa ajili ya kuzishughulikia njia hizo.
Endapo utawala wa Kizayuni wa Israel utaanzisha uchokozi na uvamizi dhidi ya Lebanon utaibua moto mkali wa makabiliano makali kati yake na Hizbullah.

THUBUTUUU ISRAEL ATAKUA HAJIPENDI ETI AINGIE LEBANON
 
Hezbolla wapo vizuri ila sio kuizidi israel na israel wakitaka kuvamia lebanon wajiandae vizuri japo kwa sasa israel imeadvance sana ..

Hezbolla wanatumia nguvu nyingi, israel wanatumia hightech.
 
Hezbollah ni kiboko kuna mwaka waligombaniana maiti moja ya mwanajeshi waliitunza wao Israel alidai anaweza kuichukua kimabavu Hezbollah waligoma vikaanza vita mpaka ikatokea wanaheshi wa Israeli wanakufa tuu huku pia idadi ya Hezbollah wakiendelea kufa mpaka kufikia mia nane naa ikabidi wasitishe wakubaliane wakarudishiana maiti zote pamoja na ile ya mwanzo Egypt ndie aliesimamia hilo naamini hawatapigana karibuni tena na ukizingatia Iran katoa msaada mkubwa kwa hao Hezbollah kwa kipindi cha karibuni na ndio maana Israel anamchukia sana Irani...
 
Mleta uzi hebu punguzaga kiherehere cha mahaba na magaidi juz ulikuja hapa na uzi kuwa Israel anashambulia tunnel Lebanon leo unakuja na uzi hizbullah ana makombola yanayofika popote ndani ya israel sharti tu Israel ashambulie Lebanon waiharibu Israel swali? Juz Israel alikuwa anashambulia tunnel wap au zile tunnel zipo upande gani...?
 
Hezbolah wamemtia israel adab lini? Israel ameanza nao vita since miaka ya 90 labda walishinda battle lakin sio war. Wanasafar ndefu ya kuiangysha israel
Hizbullah wamemtia Israel adabu vita vya 2006 ndio maana Israel hawathubutu kuvamia Lebanon. Zaidi Hezbollah ya 2018 inayo wapiganaji wamekomazwa na vita kumpigania Assad Syria.
 
Mleta uzi hebu punguzaga kiherehere cha mahaba na magaidi juz ulikuja hapa na uzi kuwa Israel anashambulia tunnel Lebanon leo unakuja na uzi hizbullah ana makombola yanayofika popote ndani ya israel sharti tu Israel ashambulie Lebanon waiharibu Israel swali? Juz Israel alikuwa anashambulia tunnel wap au zile tunnel zipo upande gani...?

Nyie watu wa ajabu sana, nani sasa gaidi? Kwahiyo israel anaeuwa watu sio gaidi!!
 
Naongezea tu kidogo.
Katika vile vita vya Israel na Hezbollah vya mwaka 2016, ni kwamba Hezbollah waliwateka wanajeshi wawili wa Israel waliokuwa wamevuka mpaka na kuingia ardhi ya Lebanon. Hezbobollah waliwachakaza hao wanajeshi wa Israel kwa Risasi zisizokuwa na idadi.
Israel wakataka kuwachukua hao wanajeshi(maiti) wao kwa nguvu, ndipo Hezbollah walipotaka wabadilishane wafungwa, kwani kulikuwa na wafungwa wengi wa Lebanon huko Israel.
Kwa mara ya kwanza Israel waliyagomea masharti hayo ya Hezbollah kwa kudhani kuwa, wao ndio wenye nguvu kwa hiyo wangeweza kuwatandika Hezbollah kwa siku mbili tu kisha wakawachukua askari wao. Kwa bahati mbaya kwa Israel, upepo ulivuma vibaya sana.
KICHAPO walichokipata Israel kutoka kwa Hezbollah kilikuwa ni cha pekee tangu Israel ianze kupigana vita na mataifa mbalimbali Duniani.
Kwa KICHAPO hicho, hatimaye Israel WALISALIMU AMRI na kukubali kubadilishana wafungwa wengi wa Lebanon walio hai na Maiti mbili za wanajeshi wao.
Hezbollah ni kiboko kuna mwaka waligombaniana maiti moja ya mwanajeshi waliitunza wao Israel alidai anaweza kuichukua kimabavu Hezbollah waligoma vikaanza vita mpaka ikatokea wanaheshi wa Israeli wanakufa tuu huku pia idadi ya Hezbollah wakiendelea kufa mpaka kufikia mia nane naa ikabidi wasitishe wakubaliane wakarudishiana maiti zote pamoja na ile ya mwanzo Egypt ndie aliesimamia hilo naamini hawatapigana karibuni tena na ukizingatia Iran katoa msaada mkubwa kwa hao Hezbollah kwa kipindi cha karibuni na ndio maana Israel anamchukia sana Irani...
 
Naongezea tu kidogo.
Katika vile vita vya Israel na Hezbollah vya mwaka 2016, ni kwamba Hezbollah waliwateka wanajeshi wawili wa Israel waliokuwa wamevuka mpaka na kuingia ardhi ya Lebanon. Hezbobollah waliwachakaza hao wanajeshi wa Israel kwa Risasi zisizokuwa na idadi.
Israel wakataka kuwachukua hao wanajeshi(maiti) wao kwa nguvu, ndipo Hezbollah walipotaka wabadilishane wafungwa, kwani kulikuwa na wafungwa wengi wa Lebanon huko Israel.
Kwa mara ya kwanza Israel waliyagomea masharti hayo ya Hezbollah kwa kudhani kuwa, wao ndio wenye nguvu kwa hiyo wangeweza kuwatandika Hezbollah kwa siku mbili tu kisha wakawachukua askari wao. Kwa bahati mbaya kwa Israel, upepo ulivuma vibaya sana.
KICHAPO walichokipata Israel kutoka kwa Hezbollah kilikuwa ni cha pekee tangu Israel ianze kupigana vita na mataifa mbalimbali Duniani.
Kwa KICHAPO hicho, hatimaye Israel WALISALIMU AMRI na kukubali kubadilishana wafungwa wengi wa Lebanon walio hai na Maiti mbili za wanajeshi wao.

Mkuu upo sahihi nakumbuka hiyo sentensi ya kuwa tutawachaka Hezbollah kwa siku mbili walipeleka vifaru vya kutosha sema Hezbollah kama Wasomari wana roho ngumu na majasiri...
 
Naongezea tu kidogo.
Katika vile vita vya Israel na Hezbollah vya mwaka 2016, ni kwamba Hezbollah waliwateka wanajeshi wawili wa Israel waliokuwa wamevuka mpaka na kuingia ardhi ya Lebanon. Hezbobollah waliwachakaza hao wanajeshi wa Israel kwa Risasi zisizokuwa na idadi.
Israel wakataka kuwachukua hao wanajeshi(maiti) wao kwa nguvu, ndipo Hezbollah walipotaka wabadilishane wafungwa, kwani kulikuwa na wafungwa wengi wa Lebanon huko Israel.
Kwa mara ya kwanza Israel waliyagomea masharti hayo ya Hezbollah kwa kudhani kuwa, wao ndio wenye nguvu kwa hiyo wangeweza kuwatandika Hezbollah kwa siku mbili tu kisha wakawachukua askari wao. Kwa bahati mbaya kwa Israel, upepo ulivuma vibaya sana.
KICHAPO walichokipata Israel kutoka kwa Hezbollah kilikuwa ni cha pekee tangu Israel ianze kupigana vita na mataifa mbalimbali Duniani.
Kwa KICHAPO hicho, hatimaye Israel WALISALIMU AMRI na kukubali kubadilishana wafungwa wengi wa Lebanon walio hai na Maiti mbili za wanajeshi wao.
Israel ilipigwa cha mbwa koko hawatosahau kamwe ngoja tuone safari hii kama wataweza kuishinda Hezbollah
 
Maneno ya mfa maji makundi yote ya kigaidi hayaogopi kitu jiulize nini kinawazuia Hezbollah kurusha maroketi yao ndiyo utapata Majibu!
Dini yao(Hezbollah) haiwaruhusu kuanza KUmSHAMBULIA adui .
Ila wakianza kushambuliwa wanaruhusiwa kulipiza kisasi .

Ebu waambie hao manguli wa telaaviv warushe ata kokoto tu southern Lebanon
Alafu usikilizie mziki wake .
 
Back
Top Bottom