Heslb yatoa siku 21 tu....

Heslb yatoa siku 21 tu....

Adolph

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2010
Posts
895
Reaction score
346
kwa wale ambao tumemaliza katika vyuo hapa nchini na kufanikiwa kupata mikopo kupitia heslb, HESLB wametoa siku 21 tu iliyoanza tarehe 23/01/2012 ili uwe umewasilisha information zako kwao au kwa debt collectors ili waanze kula chao..kinyume na hapo wamesema watafanya haya yafuatayo...

  1. Shall be liable to legal action as per Sect. 19 (a) (1) of the HESLB Act.
  2. Shall be subjected to additional monthly Penalty of 5% p.a. on the outstanding loans, over and above the 5% that was levied earlier.
  3. Shall have his/her outstanding loan loaded with the cost of tracing that will be charged after being traced by the Debt Collection Agent of the Board.
  4. Shall be blacklisted and his/her information shall be submitted to the Credit Reference Bureaux, following which they shall be barred from access to credit facilities from all Financial Institutions.
  5. Shall be barred from securing Government scholarships or admission for Postgraduate studies in any Higher Learning Institution within and outside the country.
  6. Their details shall be submitted to the Ministry of Home Affairs, Department of Immigration and all Embassies where they will be denied approval for travelling abroad.
kwa taarifa zaidi ingia hapa Loan Defaulters/Wadaiwa

nawasilisha!!!!
 
Mkwara tu huo,
Nishasema SILIPI, ule ulikua ni MSAADA uliobatizwa jina feki la MKOPO.
Hii imekula kwao.
 
sijaajiriwa wala sijajiajri...hapa wataisoma no.
 
Mbona wengine tunakatwa kila mwezi kwenye mshahara?Aisee halafu nimeona jina langu.
 
Mliopata mikopo muwe waungwana msipolipa wenzenu watasoma na nini wakati inaeleweka fika kuwa kila mwaka wanaohitaji mikopo wanaongezeka kwa kasi kuliko makuasanyo ya serikali.
 
Mbona wengine tunakatwa kila mwezi kwenye mshahara?Aisee halafu nimeona jina langu.

Mimi nilishalipa siku nyingi lakini jina lipo, naona wamechukua tu majina yote.....sidhani kama hii list iko sahihi!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hiyo orodha iko wapi labda wamenisahau wanawanee
 
Chakujiuliza je hao watu wanauwezo wa kuzirudisha?unaweza kuta walivyo sasa ni hoi kuliko walivyokuwa kipindi cha nyuma
 
Heslb hawapo makini, hawawajui wadaiwa wao, badala yake, wamechukua majina ya wanafunzi karibu yote ya wale waliosoma katika vyuo mbalimbali kwa miaka husika na kuwaweka katika matangazo; huenda labda ndiyo wanawatafuta wadeni wao, mimi nimemaliza deni langu tangu September 2010. lakini cha kushangaza nipo katika lisit. pia kuna watu ambao nawajua wamemaliza kulipa au wanaendelea kulipa lakini wapo katika lists. Wana- JF advice us, steps to be taken to Heslb for disclosing our name sas loan defaulters while we have already repaid our loans.
 
ni kweli aisee hata mimi nimebakiza mz 5 tu nimalize deni tena ghafla mwezi dec walibadili makato toka 5 hadi 15% ya mshahara lkn nipo kwenye orodha ya defaulters!
 
Mliopata mikopo muwe waungwana msipolipa wenzenu watasoma na nini wakati inaeleweka fika kuwa kila mwaka wanaohitaji mikopo wanaongezeka kwa kasi kuliko makuasanyo ya serikali.

tutalipa vipi wakati tangu tumemaliza chuo tupo mitaani hatuna ajira,wanawaajiri watoto wao,hatuna mitaji ya kujiajiri sisi ni watoto wa wakulima wanataka tulipe kimuujiza au? serikali nayo haijali inaajiri kwa kujuana,we are sick and tired tena sitaki kusikia bodi inadai hela maana hiyo mikopo kupewa tulikua tunapewa kwa mbinde tena baada ya mgomo sasa ni zamu ya bodi kugoma ili warudishiwe hela zao
 
Malipo yangu ya mkopo wachukue katika zile Mil.90 za Ester Budili.
 
Kwanini serikali isisomeshe wanafunzi bure mbona kiasi inachowapa wanafunzi ni kidogo lakini ni mzigo mkubwa kwa wanafunzi wengi wa tanzania....kwanza kwa umri wao wengi ni vijana ambao familia wanazotoka ni duni pili wengi wanaomaliza ajira hakuna zaidi ya ualimu tatu vijana wengi wanaomaliza ndo kwanza wanaanza maisha ya familia yani ya mke na mume japokua wengi wameshindwa kuoa baada ya kukosa ajira tano ata wanaobahatika kupata ajira na kufanikiwa kupata wenza wao maskini hawa vijana huanza kufikiria kupata kiwanja na kujenga apo apo ndo vifamilia vinaanza yani mtoto wa kwanza mara asaidie ndugu na jamaa mshahara wenyewe kiduchu basi ni shida tupu na nimzigo na ndomwanzo wa kutafuta njia mkato kwa vijana wetu......nashauri serikali iliangalie hili kusomesha vijana wetu hasa wa elimu ya juu wenye vigezo iwe ktk ilani na iwe ni lazima with free of charge......asilimia 95 ya viongozi wetu wa juu walisomeshwa bure kwa kodi za watanzania....better late than never..........kuwadai vijana na uku migodi waliyopewa na mungu ni laana na mwisho wake we create another tunisia.....
 
yeah am shocked mi nina karibia mwaka na ki2 naona wananikata, inamaana hayo makato ya kila mwezi kuna mwehu anakula nn.
inapain kma unalipa halafu still unaona jina lako kwenye list ya loan defaulters
 
watu watalipaje na hawana kazi
mbona wanakuwa kama hawatumiii akili,wangekuwa wanatoa na ajira ili wakidaiu wadai wakiwa wanajua kila mtu yupo ofisini
 
kulipa tutalipa ili wadogo zetu na watoto wetu wapate kusoma.tatizo hao debt collector hata siwaamini inaweza tukawa tunapeleka hela kwenye kikundi kidogo cha watu!
 
Mimi nilishalipa siku nyingi lakini jina lipo, naona wamechukua tu majina yote.....sidhani kama hii list iko sahihi!

Fuatilia Madame KH, kusanya rekodi zako zote za kuwaonyesha kwamba huna deni nao au siku za usoni wanaweza kabisa kukuadhiri. Nimeliona jina la Madame KH 🙂🙂
 
Back
Top Bottom