HESLB yapiga Ramli

encyclopaedia Tanzaree

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
513
397
Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) yapiga ramli, hicho ndicho unaweza kusema baada ya kutoa awamu ya kwanza ya majina ya waliopangiwa mikopo 2017/18 ambapo kati ya maombi 32,495, waliopangiwa mikopo ni wanafunzi 10,196.

Mkurugenzi mtendaji wa HESL amesema orodha hiyo ya wanafunzi 10,196 imepatikana baada ya kupokea na kuchambua awamu ya kwanza ya majina ya wanafunzi 32,495 waliopata udahili katika chuo kimoja.

Pia amesema kwa jumla Sh108.8 bilioni zitatolewa kwa wanafunzi 30,000 wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

Sasa swali ni je, wamejuaje kama wanafunzi 30,000 ndo watakaokuwa na uhitaji hadi mwisho wa zoezi kama bado hawajamalizia kupitia maombi yote?

Je, watakaokata rufaa watakuwa kundi lipi?

MY TAKE.
Bodi ya mikopo haitendi haki ktk utoaji wa mikopo, na hili limedhihirishwa kwa wao kutabiri idadi ya watu wenye uhitaji kabla hata hawajapitia maombi yote.
badru.jpg
 
jaman nataka kukata rufaa, msaada nifanyeje?? maana nataka kwenda chuo mwaka huu
 
Hakika Mungu mwema kwa familia yangu. Maana ilikuwa changamoto kubwa sana katika ujazaji wa maombi ya mkopo.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom