Acha ujinga mkuu, ile ni nonprofit government institution, imeundwa kwa sheria ambayo inazuia taasisi kujigeuza kuwa ya kibiashara, ipo pale kuwezesha watanzania wasio na uwezo wa kujilipia gharama za masomo ya elimu ya juu.Acha wajitangaze, wanatangaza na kutoa elimu kwa wateja wao (Wakopaji). Mbona mashirika mengi ya serikali yasiyokuwa na washindani wanajitangaza kama TANESCO, Mamlaka za maji nk.
Mikopo ndo biashara yao maana mwisho wa siku kuna riba.
Ukiniita mjinga wewe ndo utakuwa mjinga zaidi, theoretically ni sawa non profit lakini practically ni financial instution inayokopesha wanafuzi. Ndo maana wameweka na riba, vinginevyo wakiondoa riba ndo itakuwa sawa na malengo ya uundwaji wake na ndipo utaiita nonprofit.Acha ujinga mkuu, ile ni nonprofit government institution, imeundwa kwa sheria ambayo inazuia taasisi kujigeuza kuwa ya kibiashara, ipo pale kuwezesha watanzania wasio na uwezo wa kujilipia gharama za masomo ya elimu ya juu...
Inawezekana labda kuna kitu faida wanayopata kutoka kwenye tangazo hilo.HESLB ni wadhamini wa kipindi cha Powerbreakfast cha Clouds FM, swali ninalojiuliza hapa ni kwamba inakuwaje taasisi ya serikali ambayo ni non-profit institution inajigeuza kuwa profit-based institution?
Sielewi lengo lao la kujitangaza ni nini. Hawana ushindani wowote, hawana mtu wanayeshindana naye, sheria iliyounda taasisi haisemi taasisi itajihusisha na uwekezaji bali kuwakopesha wanafunzi wasio na uwezo wa kulipia gharama za masomo ya elimu ya juu.
Sasa HESLB tuambiane pesa za kudhamini vipindi vya redio mnazitoa wapi, au ndo ile 6% mnayotukata kila mwezi?
HESLB haipaswi kujitangaza la sivyo mruhusu kuwe na taasisi shindani zinazotoa mikopo ya elimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu pia.