HESLB wana tatizo gani mwaka huu?

HESLB wana tatizo gani mwaka huu?

NecZec

Member
Joined
Jan 23, 2019
Posts
68
Reaction score
118
Bodi ya mikopo ya wanafunzi mpaka leo hawajatoa majina ya wanafunzi waliobahatika kupata mkopo, iwe mkopo wote au sehemu ya mkopo.

Vyuo vinafunguliwa November mara baada ya uchafuzi mkuu tu Ila mpaka leo bado hamna majina yaliyotolewa labda kupata mkopo au sehemu ya mkopo. Wanafunzi wanahitaji kujua kama wamepata au la ili kufanya maandalizi ya namna ya kupata kiasi cha pesa kwa ajili ya usajili wa kwanza vyuoni na hata kama mwanafunzi amepata sehemu ya mkopo kujua namna gani apate hicho kiasi kingine ambacho heslb hajampa.

Si vizuri kuwashutukiza wanafunzi kwani familia nyingi vyanzo vya pesa mpaka auze mazao au mifugo.

Tuoeni majina wajue mapema.
 
Back
Top Bottom