mamabaraka
Member
- Oct 18, 2011
- 92
- 14
jaman viongozi mtaendekeza huo uozo hadi lini? Jaribuni kujisafisha japo kwa hili la ajira kwa wahitimu vyuoni, unajua sioni mantiki mwalimu na dactari anaajiliwa bila interview wengne interview mbili kuendelea ina maana matutors wa coz nyingine hawafundishi au wanafunzi hawaelewi hadi wajisomee after kumaliza chuo? Tumechoka tunataka haki. Juzi nilitafakari maisha wazazi wangu walivyokuwa wakinisihi nisome sana niwe na maisha mazuri, na jinsi walivyokuwa wanalala njaa wapate ada yangu wakiamini baadae ningewasaidia, leo hii nimeitimu chuo miaka inapita sina kazi naambuliwa kuwaomba wajinyime tena wanipe mtaji au hela yamatumizi. Inauma sana umemaliza chuo huna tofauti na aliyeishia la saba kimaisha. Siku moja nikiwa kwenye daladala alipita dada mmoja mwanasheria, teja akiwa ndani ya daladala akaanza kusema mnamcheck yule ana degree lakin ana miaka mitatu mtaani kazi hakuna kachoka hata si tunamzidi,. iliniuma hadi nikatoa machozi. Mungu atusaidie
Futeni mawazo kuwa ajira rasmi ni serikalini na taasisi zake; kila kukicha sekta binafsi inazidi kukua tafuta kampuni ndogo ukue nayo kuko BoT, NSSF, PPF, HELSB, TRA utasota sana mpaka uliowaacha mwaka wa kwanza watakukuta mtaani na ubongo umeshafuta vyote ulivyosoma chuoni. Karibu sekta binafsi ...ONYO - huku hakuna michongo zaidi ya mshahara[/QU Hujakutana na secta binafsi bro, huko nako watu tumesota unafanya kazi unasainishwa salary slip take home 700,000 unalipwa 400,000 ukisafiri per day unasain kulipwa 70,000 per day unalipa 25,000 per day,wanadai extra zinasaidia kuendesha NGO au kampuni, secta binafsi zinatusaidia kupata kazi lakini wengne wanatunyanyasa, tunavumilia maana unakuwa huna pa kukimbilia. Ila tutafika.