HESLB kwanini msiwe wa wazi zaidi?

Masiya

Masiya

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
5,101
Likes
3,425
Points
280
Masiya

Masiya

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
5,101 3,425 280
BODI imesha toa kwa kutangaza majina ya waliopata mkopo kwa awamu mbili. Hili ni sawa kabisa lakini unapotoa majina takribani 10000 kwa mfano unakuwa umeptia majina mengi zaidi, kwa nini wale ambao bodi imeamua hawatapata au wamekosa mkopo nao wasitangazwe?

Vyuo kama UDSM, SAUT vimesha waita vijana lakini kuna ambao hawajui kama wamekosa tayari hivyo bachi ya tatu ikitangazwa ndo wengine watajua kama wamekosa na maumivu kuanzia hapo. (NB: Sina account HESLB lakini kupitia hapa JF sijaona anaesema amekosa kila mtu anasubiri toleo la mwisho).

Hata tarehe wanayotegemea kutoa hiyo awamu ya tatu haijulikani. UDSM kwa mfano wanasema kama hujalipa ada (huatapata access ya boarding). Je vyuo vitapokea wanafunzi bila malipo?
 
M

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Messages
6,012
Likes
3,515
Points
280
M

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2015
6,012 3,515 280
Wanaogopa mikwara ya mkuu sijui! Ukitangaza waliokosa utakuta yatima kibao wamekosa, japo kuna waliopata ambao siyo yatima. Mwingine ukigusa tu private A level hupati mkopo kabisa japo O level ulisoma shule ya kata, na haukuchaguliwa A level serikalini. Hivyo ukatafuta private ya rahisi kama 1.5m. Likizo unafanya vibarua ili kusaidiana na mama anayetegemea mama lishe ili usome! Halafu heslb wanatafsiri kuwa una uwezo! Gharama ya Chuo kwa mwaka kwa gharama zote ni 5m, cha ajabu unakosa kabisa mkopo! Japo kuna wengine wamepata japo walisoma private!
Double standard kwa kwenda mbele!
Ukweli ni kwamba kusoma privavate si kigezo kuwa una uwezo, hatulalamiki kwa baadhi kupata japo wamesoma private, ila tunalalamika kuwa wengine wamenyimwa kwa kigezo cha kusoma private yenye gharama ndogo tu!
Ninapendekeza pia uwazi utumike kuanika majina ya waliokosa na sababu iliyopelekea wakose.
 
Masiya

Masiya

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
5,101
Likes
3,425
Points
280
Masiya

Masiya

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
5,101 3,425 280
Ninapendekeza pia uwazi utumike kuanika majina ya waliokosa na sababu iliyopelekea wakose.
Hii ingesaidia sana, unapo appeal huku hujui kwa nini ulikosa inakuwa vigumu sana kwani ni sawa na kuwa gizani. Lakini sijui kama kuna anaetusikia.
 
M

Mti mkubwa

Member
Joined
Sep 2, 2017
Messages
14
Likes
13
Points
5
M

Mti mkubwa

Member
Joined Sep 2, 2017
14 13 5
Ndugu zangu hali ni ngumu mimi kuna mdogo wangu kapata mkopo lakini kwenye mchanganuo amepewa meal and accomodation pekee ada na vitu vingine kanyimwa hivyo msubiliapo awamu ya tatu fanyeni maandalizi ya kupata pesa zaidi naamini hali hiyo itakuwa ya wengi.
 
Ndondocha mkuu

Ndondocha mkuu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2014
Messages
1,331
Likes
1,168
Points
280
Age
22
Ndondocha mkuu

Ndondocha mkuu

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2014
1,331 1,168 280
Ndugu zangu hali ni ngumu mimi kuna mdogo wangu kapata mkopo lakini kwenye mchanganuo amepewa meal and accomodation pekee ada na vitu vingine kanyimwa hivyo msubiliapo awamu ya tatu fanyeni maandalizi ya kupata pesa zaidi naamini hali hiyo itakuwa ya wengi.
mkuu huyo ashukuru sana, hiyo aliyopewa ni muhimu zaid ya adaa
 
Abdul Nondo

Abdul Nondo

Verified Member
Joined
Oct 28, 2016
Messages
111
Likes
583
Points
180
Abdul Nondo

Abdul Nondo

Verified Member
Joined Oct 28, 2016
111 583 180
*MH. MAGUFULI MIKOPO ELIMU YA JUU BADO GIZA NENE*

Anaandika.

Abdul Nondo.

Magazeti mengi,vyombo vya habari vimeandika,na watu wengi wamekuwa wakiandika baada ya kauli ya Mh.Rais juu ya kuidhinisha sh.bil 147 kwa mikopo elimu ya juu.

Ila watu wengu walikuwa wakishangilia bila jua kuwa hali ipo namna gani ,twende wote:

Bajeti iliopitishwa na bunge wizara ya elimu ikiwa na bajeti ya wanafunzi elimu ya juu mwaka huu ni sh.bil.427 (2017-2018).kwa wanafunzi mwaka wa kwanza ,wa pili ,watatu na wanne.kati ya hizo bil.427 bodi ili Fanya portion (fungu) la bil 108.8 kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza ambapo idadi iliyotengwa kutokana na kiasi cha fedha kuwa kidogo ni wanafunzi elf.30 tuu wa mwaka wa kwanza .ndio maana unaweza pata jibu kuwa idadi ya wanafunzi elf 30 kupata mkopo ilitangazwa hata kabla ya wanafunzi kuomba mkopo.

Na bodi wana kiri kuwa kati ya wanafunzi elf 61 sio elf 30 tuu ,ndio wanasifa LA hasha ,bali uhaba wa bajeti yao.

Sasa tuje katika kauli ya Raisi ya Jana kusema ameidhinisha sh.bil.147 mikopo ya juu, ni kweli Mh.Rais ameidhinisha hiyo bil.147 tangu tarehe 29 sep.2017 kwa taarifa nilizozipata ,ila sio ongezeko ni idhinisho la fedha ndani ya bajeti ile ya Bil.427 ,hivyo kiasi hiki sh.bil 147 ndio kimetoka serikali kuu ila kipo ndani ya bajeti ya bil.427,ya mikopo elimu ya juu.

Kiasi bil 427- bil 147 =280 bil.hiki kiasi cha Bil.280 ndicho bodi wameachiwa walipe ,kwa taarifa za ndani fedha za bodi makusanyo haziendi hazina ,zinabaki katika Akaunt ya bodi (EXIM BANK) Bodi wanajumuisha bil.147 iliyoidhinishwa na Rais na ile ya makusanyo ya bodi ambayo wanayo katika akaunt yao watachukua bil .280 kuongezea ,hivyo bil.147+bil.280 ya fedha kutoka mfuko wa bodi inakuwa bil.427 ya bajeti iliotengwa.

Hoja yetu nini?

Hoja yetu ni kuwa tulitegemea ufanisi,fedha kutoka serikali kuu kwenda bodi ,imepungua kwa kiasi kikubwa ,yaani mzigo wrote wameachiwa bodi ya mikopo ,serikali kuu imepunguza kiwango cha kuchangia Mikopo elimu ya juu,sababu tuu ya kuona makusanyo ya bodi .makusanyo ya bodi bado hayakidhi kuhudumia mikopo ya wanafunzi elimu ya juu,serikali kuu imeanza kujitoa kuidhinisha fedha kwenda bodi ,matokeo yake serikali inaidhinisha fedha kidogo saana ,alafu ujazo wote wa bajeti ya mikopo elimu ya juu inaachiwa bodi ya mikopo.

Miaka yote serikali kuu ndio imekuwa ikitoa fedha nyingi zaidi kwa ajili ya mikopo elimu ya juu,Takribani bil 300 hadi 400 zimekuwa zikitolewa na serikali kuu ,ambapo kama serikali kuu ingeendelea kutoa kama ambavyo imekuwa ikitoa miaka yote ,alafu tukajumuisha na makusanyo ya bodi tungekuwa na bajeti kubwa takriban bil.580 ,ingetosha kabisa kutatua tatizo la mikopo elimu ya juu.hii inafanyika Kenya Higher education loans board ,inapewa fedha yote kama ilivyotengwa na bunge ,na hutumia tena mapato yao ya makusanyo hujumuisha na kuwapa wanafunzi.

Sisi Tanzania, tunafanya Compensation (fidia) bajeti ya mikopo inatengwa kidogo,serikali inatoa kiasi kidogo ,bajeti yote inamaliziwa na bodi .

kitendo cha serikali kuu kuachia mzigo wote bodi ya mikopo na yenyewe kulipa kidogo,haileti ufanisi ,kwani itapelekea wanafunzi wengi kukosa mkopo na hivyo wengi kuhairisha masomo.

Sera ya elimu ,ya 2014 ,sehemu ya 3.3.2 ya tamko ,"serikali itaondoa vikwazo vinavyozuia fursa ya wanafunzi kuendelea na kukamilisha mzunguko wa elimu katika ngazi husika" kwa namna tuendavyo vikwazo kwa wanafunzi havitaondoka wanafunzi wengi watarudi nyumbani.

Mwalimu Kambarage J Nyerere "in education we don't have retrenchment but we have investment" we sow what we shall reap tomorrow.we shall have doctors,teachers,presidents,MPs and economists.

Katika elimu hakuna ubana matumizi ila uwekezaji ,tunapanda tutakachovuna kesho,madaktari,walimu,maraisi,wabunge na wanauchumi.

Ombi ,tunamuomba Mh.Rais ,kwa jitihada zake,tunaomba asaidie wanafunzi wafikie ndoto zao,bajeti iliotengwa ni ndogo SAA hivyo sh.bil.427 na hiki kiasi Mh.Rais ulichoidhinisha tunakuomba uongeze kidogo ,kwani kiasi kutoka serikali kuu kwenda bodi kiasi ,kimepungua saana sh.bil 147 ,tunakuomba Mh.Rais ,uwaone wanafunzi hawa ambapo wengi walioomba wanasifa waliomba elf 61 wametengwa elf 30 ,tuuu .Mh.Rais we we ni mzazi pia ,waongezee bajeti kidogo kuziba gap ili wanafunzi wengi wenyesifa wapate ila sasa hata yatima wameachwa.

Sababu bajeti haiotoshi Mh.Rais,liangalie hili.,uwasaidie hawa wanafunzi ambapo ndio viongozi wetu,umewasomesha bure sekondari ila chuo umekumbana kikwazo kitakachoziba ndoto zao.

Shukran.

Abdul Nondo.
0659366125
Abdulnondo10@gmail.com *MH. MAGUFULI MIKOPO ELIMU YA JUU BADO GIZA NENE*

Abdulnondo10@gmail.com
 
Forum statistics

Threads 1,235,696
Members 474,712
Posts 29,230,755