Heslb 2025 2026

Heslb 2025 2026

45YY

Member
Joined
Jun 24, 2025
Posts
24
Reaction score
19
NI VYETI GANI VINAKUBALIKA (BIRTH/DEATH CERTIFICATES) KATIKA KUOMBA MKOPO HESLB 2025?

Conditions Nne kwa Cheti cha Kuzaliwa;-

- Sehemu ya Entry Numbers iwe na Tarakimu tupu bila alama yoyote ile.

- Sehemu ya Child's Name iwe na Majina Matatu kwa kirefu, na sio Jina Moja au Majina Mawili.

- Sehemu ya Father's Name iwe na Majina Matatu kwa kirefu, na sio Jina Moja au Majina Mawili.

- Sehemu ya Mother's Name iwe na Majina Matatu kwa kirefu, na sio Jina Moja au Majina Mawili.

⚠️ Conditions zote hizo Nne ni LAZIMA zikubali, sio Ombi ni LAZIMA. Cheti chako cha Kuzaliwa kikikataa hata Condition moja wapo, basi utawajibika kuomba Cheti kipya cha Kuzaliwa _ (Old-To-New au Request New Certificate)_.

Conditions Mbili kwa Cheti cha Kifo cha Mzazi;-

- Sehemu ya Entry Numbers iwe na Tarakimu tupu bila alama yoyote ile.

- Sehemu ya Deceased's Name iwe na Majina Matatu kwa kirefu, na sio Jina Moja au Majina Mawili.

⚠️ Conditions zote hizo Mbili ni LAZIMA zikubali, sio Ombi ni LAZIMA. Cheti cha Kifo cha Mzazi kikikataa hata Condition moja wapo, basi utawajibika kuomba Cheti kipya cha Kuzaliwa (Old-To-New au Request New Certificate).

FOLLOW WHATSAPP CHANNEL YETU KUPATA UPDATES

👇🏽👇🏽Wazaelimu | WhatsApp Channel

NI KWANINI SEHEMU ZA MAJINA NI LAZIMA YAWE MAJINA MATATU KWA KIREFU?

Kuna wengi wenu, sio baadhi --- ni wengi, mnatumia Majina mawili tofauti kwenye Vyeti vyenu vya Elimu, Vitambulisho vyenu etc.

Kwa mfano; Eunice Careen Ibrahim, Belinda Asimwe John, Derickson Rugemalila Deusdedith, Maria Magdalena Kimaro, Mary Jane Petro, n.k. Mifano ni mingi na unaweza kuwa umeishi na hawa watu.

Ukiwatazama hao watu hapo juu, unagundua Majina mawili ya mwanzoni ni ya kwao wao wenyewe na Majina yao katikati sio ya Baba zao. Na unagundua hata the last names zao sio lazima yawe ndo majina ya ukoo.

Na sio wao tu, kuna jamii nyingine tunaishi nazo. Watoto wao wote wanachukua Majina ya Mama zao na sio Baba zao, na kuyatumia kama Last Name. Bila kusahau pia, kuna ndugu, jamaa na marafiki zetu wengi wamebadilisha Dini na automatically kubadilisha Majina yao.

Sasa watu kama hawa imekuwa ikileta Cases nyingi sana za Names Mismatch, na kwa bahati mbaya sana wengi wakawa forced kukana Majina yao na kuanza kutegemea masuala ya Viapo (Deed Poll & Affidavit of Names).

Katika kuondoa hilo tatizo, ndipo ikaonekana inapaswa kila Jina kwenye Cheti cha Kuzaliwa cha Mhusika (na/au Cheti cha Kifo cha Mzazi wa Mhusika) liwe treated separately basing na sehemu jina lilipo.

-----

Since way back, na kwa sasa, mwaka huu 2025, imewekwa emphasis zaidi;

HESLB/ZHESLB wakitaka kuangalia na/au kuthibitisha Jina la Muombaji wa Mkopo, wataangalia sehemu ya Child's Name kwenye Cheti chake cha Kuzaliwa na watafanya the same kwenye Index Number yake ya Olvl.
  • If they Do Match, hakuna tatizo.
  • If they Don't Match itaonekana umeghushi Cheti kimoja wapo, na kiroho safi watakwambia Names Mismatch ili uweke sawa hilo swala kwanza. Otherwise kaa utambue forging of Certificates ni case nzito kisheria.

Kwa Waombaji Mkopo ambao Wazazi Wapo Hai;

HESLB/ZHESLB wakitaka kuangalia na/au kuthibitisha Jina la Baba wa Muombaji wa Mkopo, wataangalia sehemu ya Father's Name kwenye Cheti cha Kuzaliwa cha Muombaji na watafanya the same kwenye sehemu ya Father's Details iliyopo ktk Fomu ya Muombaji.
  • If they Do Match, hakuna ttz.
  • If they Don't Match itaonekana Muombaji ameghushi Cheti cha Kuzaliwa, na kiroho safi watakwambia Names Mismatch ili uweke sawa hilo swala kwanza. Otherwise kaa utambue forging of Certificates ni case nzito kisheria.

HESLB/ZHESLB wakitaka kuangalia na/au kuthibitisha Jina la Mama wa Muombaji wa Mkopo, wataangalia sehemu ya Mother's Name kwenye Cheti cha Kuzaliwa cha Muombaji na watafanya the same kwenye sehemu ya Father's Details iliyopo ktk Fomu ya Muombaji.

  • If they Do Match, hakuna tatizo.
  • If they Don't Match itaonekana Muombaji ameghushi Cheti cha Kuzaliwa, na kiroho safi watakwambia Names Mismatch ili uweke sawa hilo swala kwanza. Otherwise kaa utambue forging of Certificates ni case nzito kisheria.

Kwa Waombaji Mkopo ambao Wazazi Wametangulia Mbele za Haki;

HESLB/ZHESLB wakitaka kuangalia na/au kuthibitisha Jina la Baba wa Muombaji wa Mkopo, wataangalia sehemu ya Father's Name kwenye Cheti cha Kuzaliwa cha Muombaji na watafanya the same kwenye sehemu ya Deceased's Name iliyopo ktk Cheti cha Kifo cha Baba wa Muombaji.
  • If they Do Match, hakuna tatizo.
  • If they Don't Match itaonekana Muombaji ameghushi Cheti kimoja wapo, na kiroho safi watakwambia Names Mismatch ili uweke sawa hilo swala kwanza. Otherwise kaa utambue forging of Certificates ni case nzito kisheria.

HESLB/ZHESLB wakitaka kuangalia na/au kuthibitisha Jina la Mama wa Muombaji wa Mkopo, wataangalia sehemu ya Mother's Name kwenye Cheti cha Kuzaliwa cha Muombaji na watafanya the same kwenye sehemu ya Deceased's Name iliyopo ktk Cheti cha Kifo cha Mama wa Muombaji.
  • If they Do Match, hakuna ttz.
  • If they Don't Match itaonekana Muombaji ameghushi Cheti kimoja wapo, na kiroho safi watakwambia Names Mismatch ili uweke sawa hilo swala kwanza. Otherwise kaa utambue forging of Certificates ni case nzito kisheria.

-----

From the above explanations, unaweza kuona ni kwa namna gani kila Sehemu zote zenye Majina zilizopo kwenye Cheti chako cha Kuzaliwa na/au Cheti cha Kifo cha Mzazi, zinavyotakiwa kuwa treated separately with all due respects.

Tunaomba forward huu ujumbe kwa ndugu, jamaa, marafiki na wazazi. Thank you! 🙏🏿👊🏿
 
Back
Top Bottom