wiseboy.
JF-Expert Member
- Aug 11, 2014
- 2,932
- 4,534
Naomba tujadili kwa hekima,tutoe ushabiki wa vyama tuzungumzie uhalisia.
Inasikitisha sana Rais wa nchi kupokea ndege ambayo imetengenezwa nchi nyingine ,kiprotokoli ilitakiwa ndege ipokelewe na mkuu wa mkoa au waziri husika,rais ni mtu mkubwa mno,chini yake kuna makamu wa rais,kuna waziri mkuu,kuna mawaziri kibao tu,rais ni mfalme.
Tumeonekana taifa la ma primitives,a none vision nation,taifa lisilo na maono mazito ya maendeleo baadae.
Bado hadi leo tunashangaa ndege? Ndege ni basi tu,ni barabara yake ni angani,ndege ni basi la angani,hakukuwa na sababu ya rais wetu kujichora kwenda kupokea ndege utadhani tunasindikiza wanaanga wanaoenda sayari ya mars kwa teknolojia yetu wenyewe.
Kitendo ch Rais kupokea ndege na kuizindua ina maana hatuna mkakati wowote wa kuja kutengeneza ndege zetu wenyewe.
Hatuwezi kufurahia kununua ndege badala ya kutengeneza ndege zetu wenyewe,kwa hiyo hakuna heshima ya kununua ndege,heshima ni kutengeneza zetu wenyewe.
Kama kweli tumeamua kusonga mbele kimaendeleo,basi Elimu iwe bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu,serikali iwekeze nguvu zake zote kwenye Elimu kuliko chochote,na pia iunde kitengo cha kijasusi kwa ajili ya kuiba teknolojia mbalimbali kutoka mataifa yaliyoendelea.
Vinginevyo tutaendelea kununua pamba za masikio na sindano kutoka china hadi mwisho wa dunia.
Miaka zaidi ya 50 ya kujitawala kwetu tumeshindwa hata kutengeneza pikipiki zetu wenyewe?
Yaani sisi ni dampo la kutupia kila kitu kutoka mataifa ya viwanda.
Bila mkakati wa Elimu bora na wizi wa teknolojia kama walivyofanya China na India,tutabakia hivi hivi tukila ugali na mbilimbi huku bado tukiendelea kushangaa ndege.