Heshima ya nchi ni viwanda vya ndege na si kununua ndege

wiseboy.

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
2,933
4,533
Naomba tujadili kwa hekima,tutoe ushabiki wa vyama tuzungumzie uhalisia.
Inasikitisha sana Rais wa nchi kupokea ndege ambayo imetengenezwa nchi nyingine ,kiprotokoli ilitakiwa ndege ipokelewe na mkuu wa mkoa au waziri husika,rais ni mtu mkubwa mno,chini yake kuna makamu wa rais,kuna waziri mkuu,kuna mawaziri kibao tu,rais ni mfalme.

Tumeonekana taifa la ma primitives,a none vision nation,taifa lisilo na maono mazito ya maendeleo baadae.

Bado hadi leo tunashangaa ndege? Ndege ni basi tu,ni barabara yake ni angani,ndege ni basi la angani,hakukuwa na sababu ya rais wetu kujichora kwenda kupokea ndege utadhani tunasindikiza wanaanga wanaoenda sayari ya mars kwa teknolojia yetu wenyewe.

Kitendo ch Rais kupokea ndege na kuizindua ina maana hatuna mkakati wowote wa kuja kutengeneza ndege zetu wenyewe.

Hatuwezi kufurahia kununua ndege badala ya kutengeneza ndege zetu wenyewe,kwa hiyo hakuna heshima ya kununua ndege,heshima ni kutengeneza zetu wenyewe.

Kama kweli tumeamua kusonga mbele kimaendeleo,basi Elimu iwe bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu,serikali iwekeze nguvu zake zote kwenye Elimu kuliko chochote,na pia iunde kitengo cha kijasusi kwa ajili ya kuiba teknolojia mbalimbali kutoka mataifa yaliyoendelea.

Vinginevyo tutaendelea kununua pamba za masikio na sindano kutoka china hadi mwisho wa dunia.

Miaka zaidi ya 50 ya kujitawala kwetu tumeshindwa hata kutengeneza pikipiki zetu wenyewe?

Yaani sisi ni dampo la kutupia kila kitu kutoka mataifa ya viwanda.
Bila mkakati wa Elimu bora na wizi wa teknolojia kama walivyofanya China na India,tutabakia hivi hivi tukila ugali na mbilimbi huku bado tukiendelea kushangaa ndege.
 
Una point ingawa wengine hawataiona ...........!!

Ila Elimu bora siyo lazima iwe bure. Kushuka kwa elimu Tanzania kumechangiwa sana na utumiaji wa lugha mbili katika elimu yetu (Kiswahili na Kingereza). Kama tutaendelea hivi, basi ufahamu wa vijana wetu bado utaendelea kuwa nusu nusu. Ni muda umefika sasa kuamua lugha gani itumike kufundishia watoto wetu.
 
ama kweli tumeamua kusonga mbele kimaendeleo,basi Elimu iwe bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu,serikali iwekeze nguvu zake zote kwenye Elimu kuliko chochote,na pia iunde kitengo cha kijasusi kwa ajili ya kuiba teknolojia mbalimbali kutoka mataifa yaliyoendelea.
Mkuu kila jambo linaenda kwa HATUA...miaka 20 iliyopita ELIMU YA MSINGI ILIKUWA NI LAZIMA ULIPIE...ikaja ikawa bure ikabaki sekondari leo hii SECONDARI NAYO NI BURE...kesho itakuja form five na six BURE, KESHO KUTWA chuo itakuwa ni bure pia...SO ACHENI KULALAMIKA ILI MRADI MMELALAMIKA......
 
Nimesoma hapa JF kwamba aliwaita Waandishi wa Habari Mwenyewe..Waende Wakapige picha..Na Watu waingie kwa Zamu kupiga Picha..
Ni Ushamba tu..
Hizo Tambo Anazotoa utadhani pesa imetoka Mfukoni Kwake..Kumbe ni Kodi za Watanzania Wakiwemo hao Wapinzani anaowasema Kila Wakati..
 
Kuna viwanda bila Umeme nafuu..

Bidhaa itakayozalishwa kwa gharama kubwaa mtauza wapi?

Wewe unafikiri kwa nini Sukari ya Brazil au Pakistani ni rahisi kuliko ya Mtibwa au TPC

Mafuta kupikia ya Kenya ni rahisi kuliko Alizeti ya Singida?

Mafuta ya Kenya kusafiri kote mpaka Tz halafu yauzwe sawa?

Viwanda ni Bla bla bla tu

Kodi nyiingi na umeme ghali...kuna Kiwanda gani?
 
Onyesha njia kwanza,tuone, anza na kiwanda cha sindano tu. Hapo ndipo, utaweza kuzungumzia kiwanda cha ndege na kusika vema. Wengi tumejaliwa ufundi wa meno lakini wa vitendo wanahesabika.
 
Sizonje ni aina ya watu wanaoamini utajiri ni kwenda sokoni na kununua redio kuuuubwa kisha majirani wamkome kwa kufungulia mziki mzito kwa sauti. Kwa kifupi ni limbukeni
 
Naomba tujadili kwa hekima,tutoe ushabiki wa vyama tuzungumzie uhalisia.
Inasikitisha sana Rais wa nchi kupokea ndege ambayo imetengenezwa nchi nyingine ,kiprotokoli ilitakiwa ndege ipokelewe na mkuu wa mkoa au waziri husika,rais ni mtu mkubwa mno,chini yake kuna makamu wa rais,kuna waziri mkuu,kuna mawaziri kibao tu,rais ni mfalme.

Tumeonekana taifa la ma primitives,a none vision nation,taifa lisilo na maono mazito ya maendeleo baadae.

Bado hadi leo tunashangaa ndege? Ndege ni basi tu,ni barabara yake ni angani,ndege ni basi la angani,hakukuwa na sababu ya rais wetu kujichora kwenda kupokea ndege utadhani tunasindikiza wanaanga wanaoenda sayari ya mars kwa teknolojia yetu wenyewe.

Kitendo ch Rais kupokea ndege na kuizindua ina maana hatuna mkakati wowote wa kuja kutengeneza ndege zetu wenyewe.

Hatuwezi kufurahia kununua ndege badala ya kutengeneza ndege zetu wenyewe,kwa hiyo hakuna heshima ya kununua ndege,heshima ni kutengeneza zetu wenyewe.

Kama kweli tumeamua kusonga mbele kimaendeleo,basi Elimu iwe bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu,serikali iwekeze nguvu zake zote kwenye Elimu kuliko chochote,na pia iunde kitengo cha kijasusi kwa ajili ya kuiba teknolojia mbalimbali kutoka mataifa yaliyoendelea.

Vinginevyo tutaendelea kununua pamba za masikio na sindano kutoka china hadi mwisho wa dunia.

Miaka zaidi ya 50 ya kujitawala kwetu tumeshindwa hata kutengeneza pikipiki zetu wenyewe?

Yaani sisi ni dampo la kutupia kila kitu kutoka mataifa ya viwanda.
Bila mkakati wa Elimu bora na wizi wa teknolojia kama walivyofanya China na India,tutabakia hivi hivi tukila ugali na mbilimbi huku bado tukiendelea kushangaa ndege.

Hata vikijengwa viwanda vya rocket mtakuja hapa kulalamika. Watanzania hatuna jema, mvua shida, jua kero!
 
Kuna viwanda bila Umeme nafuu..

Bidhaa itakayozalishwa kwa gharama kubwaa mtauza wapi?

Wewe unafikiri kwa nini Sukari ya Brazil au Pakistani ni rahisi kuliko ya Mtibwa au TPC

Mafuta kupikia ya Kenya ni rahisi kuliko Alizeti ya Singida?

Mafuta ya Kenya kusafiri kote mpaka Tz halafu yauzwe sawa?

Viwanda ni Bla bla bla tu

Kodi nyiingi na umeme ghali...kuna Kiwanda gani?

Wewe umefanya nini zaidi ya blah blah?
 
Wewe umefanya nini zaidi ya blah blah?

Nafanya kazi na Nalipa Kodi

Viongozi ndio wanakula Kodi zetu,,,Lazima tuhoji

Viongozi wanalipwa kwa kodi zetu waache bla bla

Eboooo...Hujui wajibu wako?

Nalipa Kodi ya PAYE Na VAT weewe....

Hujitambui eee
 
Onyesha njia kwanza,tuone, anza na kiwanda cha sindano tu. Hapo ndipo, utaweza kuzungumzia kiwanda cha ndege na kusika vema. Wengi tumejaliwa ufundi wa meno lakini wa vitendo wanahesabika.
Jamaa mshamba tu. Hana hata kijiwe cha makochi anaongelea ndege
 
Nafanya kazi na Nalipa Kodi

Viongozi ndio wanakula Kodi zetu,,,Lazima tuhoji

Viongozi wanalipwa kwa kodi zetu waache bla bla

Eboooo...Hujui wajibu wako?

Nalipa Kodi ya PAYE Na VAT weewe....

Hujitambui eee
Hiyo kodi shs ngapi?
 
Ati kupokea ndege ,ndege ya kutengenezewa?,tz haiwezi kuwa nchi ya viwanda kama chupi bado tunaagiza kutoka China?,
 
Tatizo nyie mlisema haitakuja. Sasa nimeireta kwa nini nisiizindue? Halafu wewe! Kamanda rosi kamata huyo muchochezi mufungulie mashitaka ya uchamade huyo akae miezi sita jera
 
Mkuu kila jambo linaenda kwa HATUA...miaka 20 iliyopita ELIMU YA MSINGI ILIKUWA NI LAZIMA ULIPIE...ikaja ikawa bure ikabaki sekondari leo hii SECONDARI NAYO NI BURE...kesho itakuja form five na six BURE, KESHO KUTWA chuo itakuwa ni bure pia...SO ACHENI KULALAMIKA ILI MRADI MMELALAMIKA......
Hiyo bure ni siasa za kutafutia kura,unawezaje kufanya bure huku shule zikibaki na matatizo lundo? Kuna shule nyingi ambazo hazina vyoo vyakueleweka,hamna maji,hamna umeme,hamna sakafu,hakuna vifaa vya michezo,hamna maktaba,hamna maabara,hamna viwanja nk
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom