Heshima kwako kaka pj

Jayfour_King

JF-Expert Member
Nov 15, 2009
1,135
128
Kwako kaka PJ,
Kutokana na eneo ulilopo kijiografia wewe utakuwa miongoni mwa watu wanaoweza kututhibitishia kutokana na ushuhuda mbali mbali unaotolewa na wakazi wa huko kuhusu tiba ya ki imani inayotolewa na babu huko Loliondo.

Nimekuwa nikisikia shuhuda mbali mbali kutoka kwa watu tofauti kuhusu uwezo wa dawa inayotolewa na babu Ambilikile.

Sababu inayonifanya nikuchague kama ripota ni ukaribu na eneo tiba inakopatikana na uwezekano mkubwa wa watu wengi katika maeneo uishiyo kuwa wamekwenda kupata kikombe kutokana na ukaribu wa ki eneo.

Wengine huku tulipo tunatamani sana kuwa miongoni mwa wateja wa babu lakini sababu za ki uchumi na ki jiografia zinatukaba, nategemea kusikia kutoka kwako.

Kwa heshima na taadhima,

Nawasilisha kwako.
 
Back
Top Bottom