Hesabu hizi ni sahihi: 1+1= 11; 73-3=7? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hesabu hizi ni sahihi: 1+1= 11; 73-3=7?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mtoboasiri, Aug 5, 2012.

 1. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]Na Salehe Mohamed
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="align: center"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [TABLE]
  [TR]
  [TD] LEO ninapenda kutoa ushauri wa bure kwa walimu wote hapa nchini hasa wale walioamua kugoma siku tano zilizopita wakiishinikiza serikali iwalipe malipo manono yanayoendana na ugumu wa kazi wanayoifanya.


  Walimu wanadai nyongeza ya mishahara ya asilimia 100; posho ya kufundishia ya asilimia 55 ya mishahara kwa walimu wa sayansi na asilimia 50 kwa walimu wa sanaa na wanadai posho ya mazingira magumu ya kazi ya asilimia 30 ya mishahara yao.
  Mazungumzo baina ya serikali na walimu juu ya nyongeza hizo yalikwama, walimu wakaamua kufanya mgomo uliodumu kwa siku nne.


  Ulianza Julai 30 mpaka Agosti 2, mwaka huu pale Mahakama Kuu kitengo cha Kazi kilipoamua kuubatilisha kwa madai ya kutofuata sheria zinazotakiwa.
  Kabla ya hukumu hiyo, Rais Jakaya Kikwete alitamka wazi kuwa mgomo huo ni batili na madai yao hayatekelezeki kwa sababu serikali italazimika kutumia zaidi ya sh tilioni 6.5 kwa mwaka kulipa mishahara yao tu wakati ina uwezo wa kukusanya sh trilioni 8 kwa mwaka.


  Rais Kikwete anasema, anawathamini na kuwajali walimu kwa sababu bila wao, yeye asingefikia hapo alipo.


  Kiongozi wetu ana maneno matamu, lakini hayaonekani kwa vitendo.
  Binafsi, sina hakika kama serikali inawajali na kuwathamini walimu kwa kiwango kinachotakiwa, lakini pia naamini kazi wanayoifanya ni ngumu sana inayohitaji moyo wa uvumilivu na jitihada kubwa sana.


  Bila walimu hakuna daktari, mwandishi wa habari, mhandisi, rubani na mataalamu yoyote yule. Leo hii mazingira ya kufanyia kazi ya mwalimu, ni mabaya zaidi kuliko ilivyokuwa wakati wa ukoloni ambapo idadi kubwa ya walimu walijengewa shule jirani na maeneo wanayofanyia kazi.


  Serikali yetu inasema, haina uwezo wa kulipa mishahara minono kwa walimu kwa sababu inakusanya sh trilioni 8 kwa mwaka na mishahara inayotakiwa na walimu itatafuna zaidi ya trilioni 6.5. Lakini, serikali haitaki kuzungumzia hoja ya lini itawajengea walimu nyumba kama ilivyokuwa enzi za wakoloni.


  Haisemi lini itapeleka vitabu, vifaa bora ya maabara katika shule mbalimbali hapa nchini hasa zile za ‘Kata' ambazo kila mwaka zenyewe ndizo zinazoshika nafasi za kwanza kutoka chini katika matokeo ya mitihani ya kitaifa zikizibeba shule binafsi za zile za mtakatifu fulani. Walimu wamechoshwa na mishahara midogo na mazingira mabovu wanayofanyia kazi, wanataka nyumba nzuri, usafiri na mishahara minono kama ilivyo kwa wabunge, mawaziri na watendaji wengine wa serikali ambao wanaishi kama vile wapo peponi. Serikali inapuuza kilio chao kwa kisingizio cha kutokuwa na fedha.


  Hivi serikali ina mpango gani katika suala zima la kupanua wigo wa makusanyo ya fedha katika rasilimali tulizonazo ili iongeze fedha kwa wafanyakazi wake?
  Ninasema hivi kwa kuzingatia kuwa, Tanzania tumejaaliwa kuwa na madini ya almasi, dhahabu, Tanzanite, gesi, mbuga za wanyama, milima, mito, bahari na nyinginezo nyingi tu, mbona tu maskini?


  Nawaomba walimu wasimalize hasira zao za kuzuiwa kuendelea na mgomo kwa kutowafundisha vizuri vijana wetu ili wafeli katika mitihani yao kwenye ngazi mbalimbali. Wanafunzi hawa hawajawakosea walimu, hivyo hawapaswi kuadhibiwa kwa kosa wasilotenda. Idadi kubwa ya viongozi, wanasiasa na watendaji wa ngazi za juu serikalini, huwasomesha watoto wao kwenye shule za kulipia fedha nyingi zilizopo ndani na nje ya nchi.


  Watoto wa vigogo hawajui kukaa chini kwa sababu ya ukosefu wa madawati, hawajui kusoma chini ya mwembe kwasababu ya uhaba wa madawati, hawajui michango ya ujirani mwema, wanasikia kuna wanafunzi wanakwenda shule bila viatu na hawali chakula mashuleni mwao.
  Adhabu ya mgomo wa walimu, si stahiki kwa watoto wa maskini aombaye kila kukicha, wamekuwa wakiisaka elimu kwa udi na uvumba ili wazisaidie familia zao kuondokana na umaskini hapo baadaye.
  Nawashauri walimu waiadhibu serikali katika sanduku la kura ambapo wao ndio huchukuliwa kusimamia chaguzi mbalimbali. Baadhi yao ndio hutumiwa kuchakachua matokeo hasa maeneo ambayo chama tawala kinaonekana kuanguka.
  Walimu ndio wengi kwenye ajira serikalini na ndio mtaji mkubwa wa kura kwa chama tawala kila unapofika wakati wa uchaguzi. Hivyo, walimu wakigoma kukichagua, naamini watakuwa wameitumia vizuri haki yao ya kugoma badala ya kuwaadhibu wanafunzi. Nina hakika walimu wakipanga na kufanya mgomo wa kutokichagua chama tawala, hakuna mahakama itakayoweza kuzuia mgomo huo kwa sababu utakuwa umefuata sheria na haki za binadamu ambazo zinaweka wazi kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa.


  Walimu ndio wanaotumiwa na serikali katika zoezi la kuhesabu watu na makazi (sensa), wanaweza kuligomea zoezi hilo na hapo nina hakika serikali itawasikiliza na kuwatimizia matakwa yao hata kama haitakuwa kwa asilimia 100, lakini angalau inaweza kuwa kwa asilimia 30-50. Nasema hivyo kwa kuwa serikali inawaamini zaidi walimu katika masuala muhimu kwa taifa, lakini si kuwajali na kuwathamini katika kazi zao za kila siku.


  Tafadhali, walimu msiwafundishe watoto wetu hesabu hizi: 3x3=333, 73-3= 7, 1+1=11 wala msiwafundishe wanafunzi wenu kuwa binadamu wa kwanza ni hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Source: Tanzania Daima Jumapili, 05 Aug 2012
   
 2. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,169
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  23/3=2
   
Loading...