Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Msichana mwenye umri wa miaka 16 ameishtaki shule yake kwa kumkataza kuvaa sare za wavulana
Msichana huyo ambaye yuko katika harakati za kugeuza maumbile yake ili awe Mwanamume alisemekana kuishtaki shule ya Hereford Cathedral, chini ya sheria za usawa wa kijinsia nchini humo
Ripoti zinasema anadai Walimu walimwambia hisia zake za kutaka kugeuzwa kuwa mvulana ni za muda na wengine wakamwambia anatafuta umaarufu
Lakini kwenye mahojiano aliyofanyiwa na vyombo vya habari alisisitiza huwa hajihisi sawa anapovaa mavazi ya kike, na mamake anamuunga mkono katika kesi hiyo
Imeripotiwa kwa sasa mamake ameamua kumhamisha kutoka shule hiyo kwasababu "haiwezi kumtekelezea mahitaji yake".
Kwa upande wake, shule hiyo ilinukuliwa kukataa kuzungumzia suala hilo kwa kuwa liko mahakamani
Shule nyingi zimekabiliwa na matatizo kutokana na idadi kubwa ya wazazi wanaosaidia watoto wao kubadili jinsia zao kwani huwa wanataka pia, kwa mfano mvulana anayejigeuza msichana, atumie vyoo vya wasichana.