Heri ya kuzaliwa Beni Saanane huko uliko

Heri ya kuzaliwa jembe lets Ben Saanane hakika Albert Daud Bashite damu yako itampa mapigo kumi kwa alichokufanyia ili yeye aendelee kubaki nafasi aliyopo
 
Brigadier Isaac Maliyamungu, Tanzania tunaweza kuwa na "MALIYAMUNGU" wetu! Heri ya siku ya kuzaliwa BEN SAANANE!


Tarehe na mwezi kama wa leo, wazazi wa Ben Rabiu Focas Saanane, walipata mtoto wao, wakamkuza, wakamsomesha, wakati anakaribia kuipata PhD yake huko Netherlands, Genge la "MALIYAMUNGU" likaamua kumpoteza, hata Leo siku nyingi baadae asijulikane alipo!

Wakati tukiendelea kumkumbuka na kumlilia Ben Saanane, ambaye tulipaswa kutumia akili yake kama Taifa na sio kumpoteza, tunakumbuka maisha ya MNYAMA, kiumbe katili kutoka Uganda anaitwa Isaac Maliyamungu, jasusi na katili.

Kwanini? Kwa. Sababu tunaendelea kuamini kwamba, Tanzania sasa kuna 'genge' la kupoteza watu kwa kuwateka na hata kuwaua wasijulikane walipo, kundi hilo limepata jina la "WATU WASIJULIKANA" na kweli halijawaji kujulikana!

Moja Kati ya watu katili na jeuri waliowahi kutokea katika ulimwengu Huu. Hata boss wake (Iddi Amin Dada) alikuwa akiogopa, kwa kazi ambazo alikuwa akizifanya za kutesa kuratibu mauaji ya watu ambao walikuwa wanaupinga utawala wa AMIN!

KABLA ya kujiunga na jeshi la Uganda, alikuwa mlinzi wa geti katika kiwanda cha nguo cha Nyanza. Eneo ambalo Kissaja (ndugu wa Henry Kyemba) alikuwa Meneja (personnel Manager), alipoingia jeshini, alianza na cheo cha LUTENI (lieutenant), alipewa na Amin.

Hakuna uhakika wapi alipozaliwa, historia haituoneshi. Haijulikani alikuwa kutoka Zaire au Sudan au Uganda. Lakini kwa mbali inaelezwa alikuwa kutoka kabila la KAKWA, kutoka Zaire.

Hawa kwa Wingi wao ni waumini wa uislam, wanatoka kusini Magharibi ya Sudan, wamesambaa hadi DRC (Zamani Zaire) na hata kaskazini Magharibi ya Uganda. Inatajwa ndio kabila la Isaac Maliyamungu.

Kabla ya mapinduzi ya kijeshi ya 1971 alikuwa mfanyakazi katika kiwanda cha Nyanza, wakati wa mapinduzi, anatajwa kuteka moja ya vifaru vya kijeshi, na kuongoza mashambulizi kuelekea kuuteka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe.

Maliyamungu ndie ambaye alitupa kombora ambalo liliharibu mawasiliano ya rada katika uwanja huo, anatajwa siku hiyo katika shambulizi hilo, aliwaua mapadri wawili. Mambo hao yakamfurahisha Amin.

Baada ya mapinduzi akapandishwa cheo na kuwa LUTENI (lieutenant) Isaac Maliyamungu, ujasiri wake, ukatili wake, na hata namna alivyokuwa akitenda jeshini, uliwatia hofu hata wanajeshi wenzake, wakamuogopa. Wakubwa wake wakamuogopa. Wananchi wakapeana habari zake.

Ilifika wakati Iddi Amin akafikiri Maliyamungu anakwenda kuwa kichaa. Kuna wakati Amin alimtaka Maliyamungu akawaue askari wote katika mkoa wa Acholi, akaweka askari hao ndani ya LORI, akatoka nao nje ya mji!

Wakati anawachukua, akawaeleza anakwenda kuwapa mafunzo mapya ya kijeshi hivyo wasiogope, akawataka wapange mstari, halafu nyuma yao kuna askari walikuwa kwenye Lori, wakamiminia risasi nyingi, wote!

Francis Walugembe ambaye kwa wakati huo amewahi kuwa MEYA wa MJI wa Masaka, September 1972,Walugembe alikamatwa, akaondolewa sehemu zake za SIRI, akatembezwa mitaa yote ya Masaka, kabla ya kuuwawa kikatili.

Kuna wakati alivamia kituo cha polisi, alichodai kimetoa hifadhi kwa mtuhumiwa wake, kesho yake askari wote katika kituo hicho waliamka hospitali, kwa maumivu ya kipigo! Hapo ni Entebbe!

Maasi yakitokea aliitwa Maliyamungu kuyazima. Machafuko yoyote, Maliyamungu ndie aliitwa kutuliza ghasia. Alikuwa ndie 'JEMBE LA AMIN' akishirikiana na Robert 'Bob' Astles!

Katika utawala wa AMIN, Maliyamungu ameshiriki kuwauwa madaktari, mawaziri, wabunge, viongozi wa dini, maprofesa, matajiri wakubwa, wapinzani wa AMIN, na mbaya zaidi, Familia zao, zilikuwa zinatangulia.

AMIN anatajwa kuwa na roho ya ukatili, lakini sio ya kuua watu wasiokuwa kwenye msafara wake, anasema alikuwa anshanga watu kadhaa hawapo ofisni, akiuliza, anaelezwa, Maliyamungu kafanya kazi yake!

Iddi Amin alianza kuwaua wenzake ambao walishiriki nae mapinduzi ya kijeshi, aliwatuhumu kwa kupanga njama za kumuua, akawapiga risasi, kuwanyonga na kuwakata vichwa, akawatupa msitu wa Mabira, Mto Nile na wengi wengine sehemu za mafichoni.

Wakati General Iddi Amin Dada anatoa amri kwa gavana wa Benki kuu ya Uganda kuchapa fedha mpya na kutakiwa kuifanya Kampla kuwa Mecca, Maliyamungu alipewa majukumu mazito. Alianza kumhisi vibaya!

Maliyamungu (KAMANDA mkuu wa jeshi) alitakiwa kuivamia Zaire na wenzake, Walete madini mengi awezavyo, ili kuijenga Kampala, Barabara, nyumba nzuri, hotel, hospital, maghala ya jeshi na ndege vita za kujilinda.

Unatajwa kuwa huu ulikuwa 'mchongo' ambao Iddi Amin aliutaka, ili Maliyamungu aelekee Zaire akitambua hawezi kurejea, Maliyamungu akatonywa na msaada na 'mnyetishaji' na kuepuka mtego! Hakwenda Zaire!

Iddi Amin alipewa jina la "kijambia" kwa lugha ya Luganda ni "Jambia" au kiingereza "machete" na jina hili lilitokana na kuwauwa watu wake, Nani aliwaua? Sio mwingine, Isaac Maliyamungu, ndie 'INJINIA'

INAELEZWA, Maliyamungu baada ya Vita kupamba moto 1979 Kati ya Tanzania na Uganda, alitokomea kwenda Zaire (DRC) na hailezwi aliiwenda wapi haswa, alitokomea, wengine wanasema alikufa miaka ya 1980

Historia inatufundisha hapa, hata kama ukiwa "mbabe" na mwenye kuteka na kutesa watu ipo siku yako inakuja, ambayo utapatwa na mauti, utakosana na "boss" wako! Ipo siku!

Waliomtendea BEN SAANANE haya, wapo, wanatusoma, labda wananitazama na mimi pia, labda zamu yangu haijafika, labda sijaingia kwenye anga za "Maliyamungu", lakini ipo siku, Maliyamungu wetu nae atakufa!

Wapo ambao wanawaua watu nchi hii, wanawazika, wanawatupa porini, maiti zinaokotwa porini na mtoni na baharini, watu wanapigwa risasi hadharani, wanatekwa na kupotezwa! Wanazikwa bila postmortem, wanaitwa" wahamiaji haramu", wamefukiwa shimo moja kam mizoga!

Viongozi wa dini, wanasiasa wanatekwa na kupotezwa, wanapigwa risasi, wasomi wanapotea, waandishi wa habari wanapotea, wanamuziki wanatekwa, kwanini tusiseme TUNAE MALIYAMUNGU WETU? au kuna lugha nyingine?

Ben Saanane hajawahi kuvamia kituo cha TV/Radio kwa kutumia Bunduki, Saanane hajawahi kutukana watumishi wa halmashauri hadharani, hajawahi kujiita (mungu wa DSM) na kamwe hajawahi kumpiga Waziri mkuu mstaafu (Warioba) kipigo 'heavyweight'

Kosa la Ben Saanane kwa Maliyamungu wetu ni lipi? Kuzaliwa mwanaume? Kutokuwa alipo Maliyamungu? Kuzaliwa nchi yetu? Au kosa lake ni kumiliki AKILI zaidi ya AMIN na Maliyamungu? Kwani ni dhambi kwetu kumiliki AKILI kubwa??

Kama ilivyokuwa kwa AMIN na MALIYAMUNGU, tunayashudia makubwa, watu wenye akili kubwa wanatekwa na kuuwawa badala ya kuwatumia kujenga Taifa Lao kwa kutumia akili zao, PhD ya BEN imeishia kwenye karatasi za WAZUNGU, 'tunakumiss' baba Laura!

Wakati wazazi wa Ben Saanane wanashereka siku ya kuzaliwa kwa kijana wao, kwa machozi ya uchungu, wanalia na mishumaa ya umri wa BEN, waliomteka wanalala na familia zao na kuamka!

Kama ambavyo mwisho wa Brigedia Isaac Maliyamungu ulivykuwa, kuikimbia Uganda, hata asijulikane alipokwenda, ndivyo, DAUDI ALBERT BASHITE atakavyohitaji kutumia "chochoro" kutokea nchi Jirani, asikumbuke "shimo lake CHATU" alilomtunza BEN WETU!

Heri ya siku ya kuzaliwa Ben Rabiu Focas wa Saanane!

#MMM, Martin Maranja Masese
Mbona jibu ni simple tu mwambie Dj wa ufipa amrejeshe.
 
Kwanini? Kwa. Sababu tunaendelea kuamini kwamba, Tanzania sasa kuna 'genge' la kupoteza watu kwa kuwateka na hata kuwaua wasijulikane walipo, kundi hilo limepata jina la "WATU WASIJULIKANA" na kweli halijawaji kujulikana!
Ni woga tu kwa sasa ila litakuja 'kujulikana' maadamu huyo aliyetajwa yupo siku zaja kwao itakuwa 'kheri wangefungiwa jiwe la shingoni na kutoswa ktk kilindi cha bahari kuliko ambayo yatawakuta'.
 
Back
Top Bottom