Heri kupenda usipopendwa kuliko kupendwa usipopenda

Nyoka_mzee

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
3,695
5,522
Habari za mchana wana JF,

Tumanini langu nyote ni wazima wa afya na wale wenye mitihaani mbali mbali nawaombea kwa mola mlezi awape takhfifu.

Tukirudi kwenye mada yangu,

Stori yangu ni iko hivi, kuna saheb (rafiki ) yangu mmoja kuna siku tulibishana sana juu ya hili swala na mwisho wa siku nikwamwambia heri kupenda usipopendwa kuliko kupendwa usipo penda, hakunielewa siku hiyo na tukabishana sana matokeo nikawa kimya.

Leo kaja kanishtakia kuwa kuna mwanamke anamsumbuwa sana mpaka amefika kunywa sumu kwa ajili ya kutaka kuwa na mshikaji ila mshkaji hamtaki na imefika mahali jamaa anashindwa kuwa na mwanamke anayempenda yeye kwa sababu ya huyu wanamke.

Nikamuuliza nani sasa anapata tabu hapo?

Akajibu "mimi "ikiwa na maana yeye.

Nikamuuliza unakumbuka nilikwambiaje?

Akasema; 'uliniambia heri kupenda usipo pendwa kuliko kupendwa usipopenda '.

Nikamwambia umeona sasa maneno yangu?

Akajibu; Dah kweli ila mie sikukuelewa kama ulikuwa wamanisha katika namna hii.

Nikamjibu; Ndo hivyo jambo lolote unatakiwa uliangalie pande zote.

Swali langu kwenu je nilikosea katika hili?
 
Ni ngumu lakini ukimwona mtu yuko whatsupp on line, unatuma text inaonyesha mistari miwili ya blue, inamaana ameiona na ameisoma, lakini hajajibu, hapo fikirika kidogo,

unapiga simu inaita mpaka inakatika, siku mbili zinapita hajakwambia sababu ya kutokukupiga baada ya kuona missed call, jifikirie kidogo hapo.
 
Sawa nakubailiana na ww katika hilo

Na vipi pale unapendwa na mtu ila ww humpendi na yupo unayempenda ila huwezi kuwa naye kisa tu ya huyu unayekupenda maana kucha kutwa kukuharibia huwoni maumivu mara mbili??
 
Ni ngumu lakini ukimwona mtu yuko whatsupp on line, unatuma text inaonyesha mistari miwili ya blue, inamaana ameiona na ameisoma, lakini hajajibu, hapo fikirika kidogo,

unapiga simu inaita mpaka inakatika, siku mbili zinapita hajakwambia sababu ya kutokukupiga baada ya kuona missed call, jifikirie kidogo hapo.
Hua inauma na inachoma kama pas haijalishi huyo uliye jitolea kumsabah ni ndugu,mpenzi au rafiki
 
Kuna sehemu unaweza ona kuna maslahi kwako either unampenda mtu na anakudhamini hivyo ukijipendekeza hapo hakuna tatizo,tatizo lipo pale unapoamua kujipendekeza sehemu haupendwi wala kudhaminiwa lazima udharaulike na kusimangwa

Mfano huyo mwanamke anaempenda rafiki yako analazimisha mahusiano kwa nguvu lazima adharaulike,anatakiwa akubali ukweli kua hapendwi na hadhaminiwi
fafanua mkuu vizuri maana kuna ubashite hapo umenipitia
 
Zote hamna nafuu ni sawa na kuwa mfungwa gerezani. Huyo asiekupenda lazima atakua na ampendae hivyo usaliti nje nje na siri zako lazima zitakua zinatoka kupitia umpendae
eti mimi sielewi cjui nimekula nini walah,

unamaanisha ni heri nipende mtu ambaye hanipendi kuliko kuwa na mtu ninayempenda ila yeye hanipendi?

duuuh mbona vyote ni mtihani kwangu.
 
Zote hamna nafuu ni sawa na kuwa mfungwa gerezani. Huyo asiekupenda lazima atakua na ampendae hivyo usaliti nje nje na siri zako lazima zitakua zinatoka kupitia umpendae
ndo nilikuwa naona marue rue duuuuh hii dunia ya kupenda ni shida sana.

for me bora nisijue hanipendi ila vitendo si vitaonyesha? najua hivi vitu vipo ila please naomba tu nisijue.
 
Ndio ulikosea mkuu,
Kupenda usipopendwa tabu yake ombea isikukute,
Wewe hujajiuliza kwanini rafiki yako pamoja na tabu anazosema, hajafikiria kunywa sumu? (Aliyependwa), Lakini aliyefikiria kufanya hivyo ni mwanamke (Aliyependa).
FIKRA zangu zinaniambia UKIPENDWA usipopenda UTAONA UNASUMBULIWA Ila UKIPENDA Usipopendwa UTAUMIA.
NB:- Sasa Pima kipi kina unafuu kati ya KUSUMBULIWA na KUUMIZWA.
 
hanma nafuu kabisaaaaaa duuuuh
 
Kuna wengine wanakua wanajua kabisa hapo hapendwi ila basi tu analazimisha mahusiano au ndoa kabisa,mwisho wa siku majuto.

Mambo mengine kama siri bora usiyajue ili maisha yaendelee kuliko kuyajua na maisha yakakwama kwa kukataa tamaa na uoga.
ndo nilikuwa naona marue rue duuuuh hii dunia ya kupenda ni shida sana.

for me bora nisijue hanipendi ila vitendo si vitaonyesha? najua hivi vitu vipo ila please naomba tu nisijue.
 
Kuna wengine wanakua wanajua kabisa hapo hapendwi ila basi tu analazimisha mahusiano au ndoa kabisa,mwisho wa siku majuto.

Mambo mengine kama siri bora usiyajue ili maisha yaendelee kuliko kuyajua na maisha yakakwama kwa kukataa tamaa na uoga.
uwiiiii haswaaa na kamoyo kangu kanavyopenda kufanya kazi ya ziada ndo kwanza sitaki kujua.
 
Teh teh teh teh mapenzi hiyari,Mapenzi hisia, mapenzi makubaliano bwanaee asikwambie mtu
...... Karne kumnga'ang'ania mtu asiyekupenda shida zote za nini,,, km sehemu hujapedwa hujapedwa tu at a ungejiua bila sumu
wacha weee mashallah uko good
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom