Hereni!

Sijui, nadhani ni ngumu kupata jibu muafaka. Jaribu kufikiria kuhusu waMasaai, waMang'ati n.k. makabila ambapo kuvaa hereni ni sehemu ya urembo kwa jinsi zote!

Ila kusuka...mh!

Mkuu kama unaweza kuona wamasai wamevaa hereni inakuwaje unashindwa kuwaona wakiwa wamesuka.

mwanaume anayevaa kihereni hata simuelewi,hakuna cha utamaduni wala nini,hereni za masai na wamangati zinaeleweka na zinakubalika lkn ni tofauti ni hizi wanazovaa makaka zetu wakimjini.

mbali na hereni,mwanaume anayevaa mipete mingi,anayesuka nywele,anayefuga afro,anayeweka wave,huwa simuelewi.

kuna wakaka wanapaka wanja kwa mbali na lipgloss,kuna mmoja sasa hivi ameoa aliniombaga rangi yangu ya kucha zile colorless zile zenye rangi kama ya maji zenye kungarisha kucha,nikampa nikidhani anatania duuh sikuamin jamaa ikajipaka kweli, nilishangaa.

wakaka mkizidisha ubitozi wakijiremba mkibashiwa msilalamike.

hapo kwenye lipgloss na wanja mie ndo wananishangazaaaa, halafu bado ninabakia na mshangao hadi sasa!!!!
Sasa tudubirie wapake rangi za kuvha na kuvaa magauni, kwa kwrli kaka zetu wanapoelekea sipo kabisaaaaaaaaa

Kama ingelikuwa ni kutoa maksi, basi mwanaume akivaa hereni au kasuka nywele, mimi nampa sifuri!

Mhhhh! Madame KH! kwako ni MARUKUFU kuvaa hereni na kusuka nywele!....Yaani huangalii chochote kingine! ali mradi ana nywele za kusuka na hereni basi anapewa mzinga! na yule mwenye mkufu wa gold lakini hajasuka wala kuvaa hereni je atapewa hata pass marks za kumvusha tu? Mzima KH? mbona umepotea hivyo!? Vibaya hivyo! haya uwe na weekend njema na pia ubarikiwe kwa sana tu.

BAK, yaani kabisa..anapata sifuri. Inabidi iwepo tofauti kati yangu na yeye...sio kila asbuh tunakuwa busy wote kujiremba..hahaha!
Kwa mkufu, mhh may be anaweza kupata some maks, ila sijui hata zitafika pass mark....:)
Mi mzima kabisa BAK, mzima wewe? Nitajitahid kutopotea sana...

• Thanks
Reactions: BAK

Mhhhh! haya nimekuelewa...mimi poa kabisa namshukuru sana Muumba wetu....furahia mwisho wa wiki.

Ukiona mwanaume ana tabia kama za kike (kusuka,kuvaa hereni,kuvaa cheni either shingoni or kiunoni) NI ZUZU na anaweza kuwa na sifa za kuwa mwanamke kwa asilimia 80. KWAKWELI HUWA SIPENDI KUMWONA MWANAUME ANAKUWA NA UJINGA WA NAMNA HII.

Sifagilii kabisa mwanaume kuvaa hereni na akianza kuvaa hivyo ataanza kupaka na cream mwisho wa siku tutaanza kugombania dressing table asubuhi kujipaka powder

Ni western life style jamani!
Acha wafanye wapendavyo
Kwani au yetu au aibu yao?

Mmenikumbusha 'Chief of Protocol' wa Ikulu enzi za BWM, (aliwahi pia kugombea ubunge jimbo la Temeke kwa tiketi ya wanaojidai kujivua magamba) ni balozi wa nchi moja huko Asia, sijui bado anavaa hereni?

Hapari wapendwa!

Poleni na mihangaiko ya hapa na pale

tumekuwa tukichangia hoja za hapa na pale, zaidi kuna uzi mmoja hivi tulikuwa tukiuchangia kuhusu suala la wanawake kuvaa wigi, kila mmoja ni shahidi jinc watu walivyochangia/kupinga.

Sasa leo naomba mchango wenu kuhusu suala la wanaume kuvaa hereni na kusuka kama wadada!
Hivi hii ni akili au upunguani?
Hii ndo kwenda na muda au ndo kuchanganyikiwa?

Sio kwenda na wakati mkuu...wamasai mbona ni mila zao kusuku na kuvaa hereni wanaume? sema tu wewe upo mbele sana kufikiria...mtu afanye anapojisikia...

Hapo nakupata, sio siri element za kuchora 7 zipo, inakuaje mwanaume uvae hereni kama za dadaako, usuke nywele ka mamaako afu ujiite dume?
Tuachane na zile za asili kama za wamasai ambao huvaa hereni wakiwa ndani ya mavazi yao ya asili, sasa we haupo kwe asili afu umetoga masikio, nyusi, nk mfn Aliekuwa mtangazaji wa EATV Ben K. Sasa ile ni asili au ni nini?

Hivi Ben K mtu wangu ni mwanume yule? mbona sio elements tu za kike anazo ila full wa kike..

hakuna kitu nachukia kama mwanaume kuvaa mikufu

nachukia zaidi pale anapovaa HERENI
Halafu nachukia na kukasirika pale wanapovaa MILEGEZO
na huwa nanuna nikiona wanaume wakitembea barabarani na vikaptura mpaka "maumbile" yao yanayowasababisha kuitwa wanaume yanapojichora kama yalivyo kwenye hivyo vikaptura !!!

yaani nachukia nachukia nachukia.....
natoka kwa sasa... nitarudi kumalizia!!!!!!!!

Vipi madada wanaoweka matiti yao nje? kama hiyo avata yako?unawapenda eeeeeeeeeeeeeee

mi mzima,
hao wanaovaa pichu nje ndo natamanig niwanyuke viboko,nahis wanawatega wanaume wenzao maana unakuta wakipita wanaume wenzao wanakodolea macho.hii dunia imechefuka sana

Avatar yako mbona inanitia wehu mie? Na nyie jamani wanawake acheni kututega kuvaa nguo zinazobana makalio hujui tunaumia sisi?

Mi mwenzenu napenda mwanaume wangu akivaa cheni shingoni mara mojamoja,napenda kuichezea ikiwa hapo ILA akivaa hereni na kusuka nywele sipendi hata kuongoza naye japo kwa asili wamasai wanavaa,na kwa asili kuna makabila ni kawaida wanawake kuvaa vinguo(vingozi) vya kuacha makalio/matiti wazi.
Cha msingi ni kwamba tumeshastaarabika,tujue kujihifadhi maungo yetu(wanawake na wanaume).

Back
Top Bottom