enockino
JF-Expert Member
- Oct 14, 2014
- 273
- 171
Anaandika Diwani wa Kata ya Kongolo- Magu na Mwanafalsafa Herbert Faustine
____________________________________
MAMA JANETH USISOME ANACHOANDIKA KIGWANGALA.
Sitaki kurudia alichoandika Hamisi Kigwangala, sitaki kabisa. Kinajulikana. Kama unaweza kupata shahada ya uzamivu kwa kuandika thesis iliyoshiba na kukubalika na wakufunzi, basi pia unaweza kuwa Profesa kwa kuhitimu chuo cha ujinga na upuuzi ndani ya jamii. Tanzania tumepata Profesa wa kwanza specialised in ujinga na upuuzi.
JPM hakuwa Rais tu, alikuwa Baba wa familia, si Baba tu alikuwa mme wa Mama Janeth Magufuli. Janeth hakuwa first lady tu bali alikuwa mke wa hayati Magufuli. Alihitaji kuwa karibu na mumewe muda wote hasa mara baada ya muda wa kazi.
Siku moja usiku baada ya muda wa kazi, hayati Magufuli akamwacha mkewe akaenda kumsubiri Hamisi Kigwangala uwanja wa ndege akiwa hoi baada ya ajali..sijui huyu Mama kama ameona anachokiandika au kukisema Kigwangala.
Ukitaka kuwa mkulima wa mpunga kubali kugusa tope, Profesa Kigwangala katulazimisha tumguse. Hatukuwa na mpango nae ila kataka tujue kuwa nae yupo! Ukijampa kwa hasira utajinyea. Ukitaka umaarufu na ukaona hauji kwa mema utalazimisha kutembea uchi mana lengo ni umaarufu uwe kwa positive au negative shida ni umaarufu.
Mwaka 2015 wakati Kigwangala anachukua form ya urais kupitia Chama cha Mapinduzi alitoa hotuba yake. Hotuba ile ilikuja kugundilika kuwa kafanya wizi wa kazi ya mtu haikuwa yake. Alichokifanya Profesa Kigwangala ni kupachika majina ya wanae tu mara Hamida kwenye jina la Collins n.k.
Pamoja na wizi huo ambao nchi zilizoendelea ilikuwa kashfa ya kumfanya asiaminike popote, Kigwa aliaminiwa na kuingia kwenye baraza la mawaziri kama naibu baadae Waziri wa mali asili na utalii.
Kigwangala mwenye ushamba uliokubuhu akiwa Waziri akaanza kujiita Mzee wa nje ya boksi, mara Mzee wa fildi. Akaingiwa na ubishoo wa kuchelewa kujua mambo akachonga na fimbo kama ya Mwl. Nyerere akawa anaposti kila tukio analolifanya. Akaona haitoshi kutuonesha gari na mapori anayotembelea kwa kodi zetu huku akijigeuza mtalii yeye mwenyewe akaanza kutupa historia ya Baba yake alivyomtongoza Mama yake na alivyozaliwa. Watanzania tulikaa kimya kwa kujua kuwa kuna nyakati mtu anachelewa kubalehe akiwa kijana anabelehe akiwa mtu mzima, tukaona hili limemtokea Kigwa kama exceptional/abnormality. Tukamsamehe.
Akiwa waziri wa Mali Asili Profesa Kigwa alianza kutumia ndege za TANAPA kama bodaboda kwa matumizi yake mwenyewe. Akaanzisha na safari za akina Steve Nyerere na Shilole (kwa jina la wasanii) kupanda mlima Kilimanjaro. Kigwa aligombana na Katibu Mkuu wa wizara yake mpaka hayati Magufuli akawasema hadharani. Huyu ndiye Profesa Kigwa.
Kigwa akaanza kutusema vijana kuwa hatupendi kujiajiri! Akaanza kuweka mitandaoni mazizi yake ya ng'ombe na mashamba ya mpunga. Kigwa akatuonesha alivyo tajiri sababu ya juhudi binafsi. Maskini wa akili akipata dhihaka mtazioga kama maji.
Kujua kwamba kujiajiri ni kugumu Kigwangala akanunua baiskeli za kuhonga wajumbe wa mkutano mkuu jimboni kwake! Japo hazikugawiwa kwa maelekezo ya TAKUKURU lakini wajumbe walimpa kura haraka kabla ya saa sita mchana ili wakapate mgao wao. Akashinda.
Baada ya uchaguzi mkuu Kigwa akabwaga baraza la mawaziri. Kigwa akaehuka. Akachukua familia akaipeleka Uarabuni na kuanza kuposti picha wanae wakiwa wamepanda Ngamia na Farasi. Chini ya maneno ya picha hizi aliwananga maskini kwa kuonesha anaweza kuishi maisha mazuri hata bila uwaziri. Bado tuliendelea kumsamehe sababu ya ushamba na ulimbukeni.
Tarehe 17 March mwenyezi Mungu akamchukua John Pombe Magufuli. Katika kipindi cha maombolezo Kigwa akaja na masimulizi jinsi Rais alivyokuwa anamjali na kumsaidia kazi kipindi cha Uwaziri wake. Akasema alivyopigiwa simu na Magufuli atoke eneo ambalo si salama. Akaenda mbali zaidi kusimulia Rais alivyoisubiri ndege iliyombeba baada ya ajali. Kwenye masimulizi anasema Rais alikaa uwanjani kusubiri ndege mpaka usiku (Mama Janeth akiwa peke yake mumewe kaenda kumuona Kigwa).
Ukitazama masimulizi ya Kigwa kabla ya maziko ya JPM, ni kama kwamba alijua atafufuka na kuendeleza Urais hivyo alikuwa anasaka fursa. Ghafla akili ikamrejea kuwa JPM hatutamuona tena. Akatafuta engo ya kutafuta umaarufu ama akumbukwe na Mama Samia au tujue kuwa nae yupo.
Huko nyuma katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid-19, Kigwa aliungana na JPM na kusema upigaji nyungu ni njia ya kujikinga au kutibu ugonjwa huu. Akaenda mbali zaidi akaanza kutoa maelezo ya kitaalamu kwanini nchi isipokee chanjo.
Kigwa akiwa na akili timamu akaagiza vituo vya kupokea watalii vijenge vyumba vya kupigia nyungu. Sidhani kama hapa alishurutishwa na JPM.
Juzi Kigwa kayakana yote na kusema pale Muhimbili watoe hicho kibanda cha upigaji nyungu. Profesa Kigwa ni udhihirisho wa kwamba binadamu haaminiki.
Ukisikiliza maneno ya Kigwangala unaweza kuwaza mbali zaidi kwamba Je ile ajali ilinyofoa baadhi ya nyaya kwenye ubongo wa Kigwa? Mana kwa mwendelezo huu ipo siku anaweza kumtwanga makonde Mbunge mwenzake pale Bungeni ndiyo tujiulize imekuwaje kumbe mtu ana tatizo la siku nyingi ila tumelipuuza ila dalili zake anazionesha wazi.
Hebu pata picha Mama Janeth anapoona yanayosemwa na waliokuwa wasaidizi wa hayati mumewe. Wapo waliompigia simu JPM akiwa na mkewe nae alisikia walivyokuwa wakiongea tena wakijifanya wako karibu na JPM muda wote, Kigwa ni mmoja wao. Huyu Mama anaumia kiasi gani.
Kama kuna ukosoaji wa serikali ya Magufuli acha ufanywe na watu ambao hawakuwa sehemu ya serikali hiyo. Lakini kama mtu alikuwa Waziri, Mkuu wa mkoa, Mkuu wa wilaya kuanza, sijui Katibu wa wizara kuanza ukosoaji kwa sasa ni utafutaji fursa kwa Mama Samia na si vinginevyo.
Maana hatukuwahi kusikia mtu kaachia ngazi sababu kamshauri Rais na ushauri wake haujasikilizwa. Wote walikuwa kimya wakila na kusaza mezani pa JPM. Kigwangala ni mifano ya akiba ya kutosha ya wanafiki ambako taifa hili linao.
Mama Janeth umsamehe tu Kigwa, na sana sana huku mitandaoni si mahali pako kwa sasa! Huku utakutana na wasaidizi wa hayati mumeo wakisaka fursa kwa ukosoaji wa kilichofanywa na JPM. Kigwangala anawakilisha kundi kubwa la wanafiki ndani ya chama cha Mapinduzi. Hayati Mwl. Nyerere aliwahi onya kuhusu wanasiasa malaya! Kama mtu hajawahi elewa maana ya umalaya wa kisiasa basi mtazame Profesa Kigwangala.
Herbert Faustine
Balozi nje ya ubalozi