Hembu tupitie kisa cha Mungu jua (helios) na mwanae (phaethon)

bahati93

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
1,131
2,008
Hichi ni kisa cha kale kinachopatikana katika hekaya za zamani za waigiriki na miungu yao, iliyokuwa ikiabudiwa kipindi hicho kabla ya KRISTO.

Tofauti kubwa kati ya miungu yao na MUNGU anayeabudiwa na wakristo ni kwamba miungu yao nayo ilikuwa na hulka mbalimbali za kibinadamu tofauti ni kwamba walikuwa nguvu Zaidi ya binadamu.

Hii miungu ilikuwa na kiongozi wao aitwaye ZEUS huyu ndie aliyekuwa kiongozi na ndio aliyekuwa na nguvu kuliko wote, huyu ndiye ambaye alikaa nafasi ya MUNGU wa kikristo baada ya waroma ( warumi ) kuadopt dini aliyohubiri YESU.

Hawa waaigiriki walikuwa na miungu mbalimbali ambapo kila muungu ulikuwa na wajibu wake huyu HELIOS yeye majukumu yake yalikuwa ni kuondesha gari ya farasi waendao kasi kulivuta jua kutokea mashariki na kuzama magharibi kila siku hii ndio kazi yake kuu aliyo kuwa akifanya, kufanya usiku na mchana uwe na ukawa.

Kisa kilikuwa kwamba Phaethon mtoto wa kiume wa mungu jua alikuwa akiishi duniani kwani baba yake Helios alizaa na mwanadamu.

Huyu kijana phaethon alikuwa akikwazika kutokana na Vijana wenzake kutokubaliana naye alipowambia baba yake ni muungu HELIOS, wanamchukulia poa, na wengine kumwambia athibitishe kama kweli Helios ni baba yake.

Basi hio siku moja ilipowadia baba yake akiwa kashuka chini kuja kumsalimia akamkuta mwanae katika hudhuni akamwambia wahudhunika nini niambie kitu chochote nami nitakutendea ili nikutoe katika hudhuni, ndio Phaethon akaeleza kadhia inayomsumbua ya kutaka kudhibitisha ya kuwa yeye ni mtoto wa helio kwa kumwomba baba yake amwachie aendeshe farasi wa jua ili athibitishe, Helio alikuwa hana budi kumwachia.

Ikawa ni kasheshe mara baada tu ya phaethon kukabiziwa uskani ili aongoze farasi kwani farasi walikuwa na nguvu na spidi kali sana hali hii ilipelekea jua kwenda kwa kuyumba yumba na kusababishaa maafa ya moto dunian katika bara la Africa walichoma moto msitu eneo la kati na kusababisha jagwa la sahara na kufanya waafrika kuwa na ngozi nyeusi.

Kasheshe hio ilipelekea ZEUSI kuingilia kati kwa kurusha radi kali iliyomtungua phaethon na kumpelekea mauti kabla hajachoma dunia nzima.

Haya tuachane na stori hii tuje sasa kwa ukinzani uliopo baina ya wababa na watoto wao wa kiume kuhusu majukumu. ni jambo la kuogyofya pale mbaba anapoombwa na mwanae kuendesha gari, sasa kinini kifanyike;

Hii stori imenibidi kuleta kwenu kutokana na kisa kilichotokea mara kuendana na kisa hicho cha helios na mwanae.

Ni wajibu ya wababa kutambua kuwa watoto wao wanawaangalika katika matazamio makubwa na wanajitamba kwa wenzao kuhusu fani za baba zao hivyo basi wababa wanapaswa kufanya juhudi kushare ujuzi na watoto wao, kama una gari hakisha mara moja moja unamwachia mwanao atanue.

Sio unaleta maneno ya kuvunja moya ya “ na wewe tafuta la kwako” kwani huyo mwanao alikuomba umlete duniani kwenye vishawishi. Muhimu kushare power ambazo unazo, ni hayo.
 

Attachments

  • helio and son.jpg
    helio and son.jpg
    99.4 KB · Views: 23
Back
Top Bottom