Help with my laptop cursor

reandle

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Posts
11,166
Reaction score
8,159
Wadau na magwiji wa Jukwaa hili , salaam!
Kwa muda mrefu nakoseshwa raha na Cursor kwenye Laptop yangu! Sina uhakika ni jambo la kawaida kwa Laptop zote au ni kwangu tu! A year ago niliwahi kuleta hoja hii hapa hapa, but haikuwa na response. Nimeonelea niilete tena hoja hii.

In short, wakati nina-type, anytime without my concern, Cursor huwa ina-skip position iliyokuwapo na kwenda kabisa...sometime hata kwenye paragraph nyingine. Hii maana yake ni nini, natakiwa macho kutoyatoa kwenye screen hata sekunde moja wakati my experience in writing hainilazimishi kukodolea screen. Mbaya zaidi, inanilazimisha kuwa very slow in typing! Sina hakika kama nimeeleweka! Assume nilikuwa nataka ku-type neno "inanilazimisha kuandika." So unaweza kuta, ninapofikia kuandika
"inanilazimisha kuan...." cursor inahama na kutoka kwenye "n" na say inarudi anywhere within the word inanilazimisha to the point kwamba, kama nitakuwa naendelea ku-type, neno INANILAZIMISHA halitaendelea tena kuwa hivyo na litakuwa ni neno lisilo na maana yoyote.

So guys, kama kuna namna yoyote naweza kutatua hili tatizo, please help!

UPDATES: PROBLEM SOLVED, So thread ipotezeeni. But for anyone having similar problem, below are procedure to fix the problem:

STEPS:
Start>>Control Panel>>Mouse>>Pointer Options
After Clicking Pointer Options Tab,
Uncheck: "Hide Pointer While Typing" check box
Click: Apply>>OK.

 
Sasa kama ni kwa mwaja mzima mkuu si upige chini hilo windows kisha uweke upya au kama vipi update drivers
 
Sasa kama ni kwa mwaja mzima mkuu si upige chini hilo windows kisha uweke upya au kama vipi update drivers
Kwa sasa natumia laptop nyingine tofauti na ile ya mara ya kwanza ambayo ilikuwa inatoa similar problem!! Zote zinatumia Windows 7
 
Pole,ukiacha sababu zingine pia ukiwa unatype vidole gumba vyako inawezekana vikawa vinagusa mouse button bila wewe kujua na kufanya curse imove.Jaribu kutype kwa makini one char at a time uone je bado curse itamove,hakikisha ukiwa unatype haugusi mouse button.
Jaribu hiyo kama ikiiendelea tufahamishe ili tukupe suluhisho mbadala.
 

Mkuu wangu, tatizo wala halikuwa kugusa mouse button...kwani hata staili ya typing yangu, viganja vinakuwa mbali sana na mouse button. Hata hivyo, problem solved!
 
Mkuu wangu, tatizo wala halikuwa kugusa mouse button...kwani hata staili ya typing yangu, viganja vinakuwa mbali sana na mouse button. Hata hivyo, problem solved!

how problems solved au kwa kuwa we umejua utaki wenzako wajue
 
Mkuu wangu, tatizo wala halikuwa kugusa mouse button...kwani hata staili ya typing yangu, viganja vinakuwa mbali sana na mouse button. Hata hivyo, problem solved!

Ok.Ila bado hujasema umesolve vipi kama ulivyoulizwa solution uliyoweka hapa ni kwamba unatumia laptop mpya kama sijakosea.Tupe ujuzi utatusaidia mbele ya safari.
 
Ok.Ila bado hujasema umesolve vipi kama ulivyoulizwa solution uliyoweka hapa ni kwamba unatumia laptop mpya kama sijakosea.Tupe ujuzi utatusaidia mbele ya safari.
Umeisoma post kwa haraka....chini nimeandika UPDATES na nikaandika jinsi nilivyo-solve!! Check it out paragraph ya chini!!
 
Tatizo likiendelea mtafute mtaalam Kimox kimongole huku JF atkusaidia bureeeee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…