Said Cosmetics
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 2,007
- 1,600
Bibi mmoja alienda bank kuchukua pesa zilizokuwemo kwenye account yake, akaandika cheque na kumpa mhudumu wa benk (teller), huku akisema nataka kutoa Tshs 150,000/="
Yule mhudumu (Binti) akamwambia yule bibi kuwa mtu anayetoa chini ya laki tano (Tshs 500,000/=) yafaa awe anatumia ATM. Hivyo aondoke na kwenda kutoa hicho kiasi kwa njia ya ATM.
Yule bibi akauliza kwanini? Yule mhudumu akajibu kwa hasira akisema, Hii ni sheria, Tafadhali ondoka kama huna jambo jingine zaidi ya hilo, kunaforeni kubwa nyuma yako, tafadhali wapishe wateja wengine. Kisha yule mhudumu akamurudishia yule bibi cheque yake.
Yule bibi akabaki kimya. Kisha akairudishe ile cheque kwa yule mhudumu na kumwambia kama ndo hivyo basi naomba nipe hela zote zilizopo kwenye account yangu.
Yule mhudumu alipoingia kwenye acount ya yule bibi alishangazwa na kiasi kikubwa cha pesa zilizokuwemo kwenye account ya yule bibi.
Ndipo akasema samahani bibi, unakiasi cha Tshs milioni 500 kwenye account yako. Hii pesa ni nyingi sana, benk yetu haina kiasi hicho kwa sasa, labda utoe oda ili tukupatie kesho.
Yule bibi akauliza "kwahiyo ni kiasi gani naweza kutoa sasa?
Yule mhudumu akajibu kiasi chochote kisichozidi milioni 100.
Basi yule bibi akasema basi naomba nipe milioni 100 toka kwenye account yangu.
Yule mhudumu akafanya haraka na kutoa kiasi cha milioni 100 kisha akamkabidhi yule bibi kwa heshima kubwa.
Basi yule bibi alitenga kiasi cha Tshs 150,000/= na kuiweka kwenye mkoba wake kisha akamrudishia yule mhudumu Tshs 99,850,000/= na kumwambia airudishe kwenye account yake.
Basi yule mhudumu akabaki anatetemeka.
Unajua nini?
Sheria hazibadiliki ila sisi binadamu tunabadilika pale tunapokutana na vitu vinavyotufanya tubadilike.
Tusiwe tunawadharau au kuwaheshimu watu kwakuangalia mwonekano au mavazi yao.
Ila inatupasa sote tuishi kwa kuheshimiana. Na tusifanye haraka kukikosoa kitabu kwa kuangalia kava lake.
CHINI YA JUA KILA MMOJA WETU ANAUMHIMU.